WAFANYAKAZI KASHWASA WAONYESHA FURAHA YAO KWA KUSHEREKEA SIKU YA MEIMOSI



Na Kareny Masasy, Kahama 
MAMLAKA ya  Maji safi na Usafi Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) wameadhimisha siku ya Wafanyakazi (Meimosi)
 
Mkuu    wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo  amesema  hajapata malalamiko yoyote  kutoka kwa wafanyakazi huku akiwaomba waendelee kufanya kazi vizuri  zaidi  na mazingira yao yakiendelea kuboreshwa. 
Mhita amesema yapo mafanikio mengi yaliyopatikana kwa wafanyakazi ambapo wapo waliopandishwa madaraja na mazingira ya kazi kuboreshwa  pia changamoto walizozitoa zote ataziwasilisha mahali husika na zilizo ndani ya uwezo wa  mkoa zitafanyiwa kazi.

"Salamu mlizozitoa kwa Rais nitazifikisha na changamoto kama waajiri kutumia vibaya mikataba ya wafanyakazi wao na wengine kuzuia kujiunga na vyama vya wafanyakazi  na mfuko wa hifadhi  ya jamii (NSSF) kutopeleka michango na kuchelewesha wastaafu " amesema Mhita.

Mhita amewatoa hofu watumishi walioko ndani ya mkoa kwani maslahi yao yanaendelea kuboreshwa  ametoa rai waendelee kuwa na weledi kutambua haki  na wajibu inayoendana na waajiri.
 
Mratibu wa Shirikisho la  vyama  vya  Wafanyakazi  nchini (TUCTA) kwa mkoa wa  Shinyanga Ramadhani Pangala amesema  wafanyakazi wa sekta  binafsi  na serikali  waboreshewe  maslahi yao kwani   wanaipongeza serikali  kuzingatia  utoaji wa ajira  mpya kwa vijana. 
 
Maadhimisho  hayo yalikuwa na kauli mbiu  isemayo kazi zenye staha  ni nguzo  imara kwa Maendeleo   endelevu  katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050. 





Post a Comment

0 Comments