Na Kareny Masasy,Shinyang
Waumini wa dini ya Kiislamu wametakiwa kuendelea kuliombea taifa amani na utulivu pamoja na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake ili iweze kuliongoza vyema taifa na kuwaletea wananchi maendeleo.
Wito huo umetolewa leo Machi 21, 2026 na Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, wakati wa swala ya Eid al-Fitr lililofanyika katika viwanja vya Sabasaba mjini Shinyanga.
Amesema pamoja na kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, bado waumini wanapaswa kuendeleza matendo mema waliyokuwa wakiyafanya, ikiwa ni pamoja na kusaidia wahitaji na kudumisha mshikamano katika jamii na kuliombea amani taifa.
“Mwezi mtukufu wa ramadhani umemalizika nawaomba waislamu tuendelee kutenda mema na kuombea amani na utulivu taifa letu,”amesema Sheikh Makusanya.
Aidha, alimpongeza pia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kitendo cha huruma cha kumuasili mtoto mchanga aliyetelekezwa na mama yake mkoani Tabora, akieleza kuwa ni mfano wa kuigwa kwa Watanzania wote.
Katika hatua nyingine, aliwataka vijana wa bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa kuepuka mwendokasi na kubeba abiria kupita kiasi, ili kuepusha ajali zinazogharimu maisha.
Nao baadhi ya waumini wa dini hiyo, walisema mawaidha ambayo wamepewa na kiongozi wao watayazingatia ili kuendelea kuisha kwa amani na upendo.
0 Comments