MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro amewataka wananchi kuongeza ushirikiano na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kuimarisha haki na kuchochea maendeleo ya taifa.
Mtatiro amesema hayo katika hafla ya futari (Iftar) iliyoandaliwa juzi na TAKUKURU Mkoani Shinyanga huku akieleza mapambano dhidi ya rushwa hayawezi kufanikiwa bila ushiriki wa wananchi.
Mtatiro alisema rushwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo na husababisha upotevu wa rasilimali za taifa, huku akibainisha kuwa vitendo hivyo vinahusisha pande zote mbili—wanaotoa na wanaopokea.
“Mapambano ya rushwa yanahitaji ushirikiano wa dhati kutoka kwa wananchi ili kuhakikisha rasilimali za nchi zinasimamiwa kwa uadilifu na kunufaisha wote,” alisema Mtatiro.
Mtatiro alieleza kuwa changamoto ya ukosefu wa maadili kwa baadhi ya watumishi wa umma imekuwa ikichangia kuwepo kwa vitendo vya rushwa hali inayosababisha wananchi kunyimwa haki zao.
wananchi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwa TAKUKURU, akisisitiza kuwa taasisi hiyo imejipanga kupokea na kufanyia kazi taarifa hizo kwa ufanisi.
Mtatiro amesema TAKUKURU kwa kuendelea kutoa elimu kwa umma na kufanikisha ushiriki mkubwa wa wananchi katika hafla hiyo, akisema ni ishara kuwa jamii imeanza kuelewa umuhimu wa kupinga rushwa.
Mkuu wa Takukuru Mkoa Donasian Kessy ametoa zawadi kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu akieleza hatua hiyo inalenga kuimarisha uhusiano.
Sheikhe Mkuu wa Mkoa Ismail Makusanya alisema jambo lililofanywa na taasisi hiyo ni kubwa kuwajali waumini wa dini ya kiislamu na watoto hivyo alipongeza kwa hatua hiyo.






0 Comments