SHINYANGA YAWEKA MPANGO WA UTEKELEZAJI WA MALEZI NA MAKUZI

Na Kareny   Masasy,Shinyanga

WADAU Mkoani Shinyanga wametakiwa  kushiriki vizuri  programu jumuishi ya Taifa ya Malezi Makuzi na  Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) pamoja na Mpango Mkakati wa Mkoa wa Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (Mtakuwwa) ili kuendelea kujenga  jamii kupata kizazi kilichobora.
Hayo yamesemwa leo  kwenye kikao cha wadau  wa Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kilichofanyika  kwenye ukumbi  wa Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa kilichoratibiwa na shirika la ICS kwa kushirikiana na Mratibu wa PJT-MMMAM Mkoa  ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii  Lyidia Kwesigabo .
Kwesigabo akitambulisha  MMMAM   kwa wadau  mbalimbali amesema jukumu kubwa ni kuhakikisha watoto wanakuwa  kwa kupata nguzo tano muhimu ambazo ni Malezi yenye mwitikio,Afya bora,Lishe,Ujifunzaji wa Awali  na Ulinzi na Usalama na kumuepusha viashiashiria vya hatari ambapo mtoto anakuwa na uelewa  ubongo wake hata kabla ya kuzaliwa.

“Ndiyo maana tumelenga watoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi minane  na  wanapochangamana na watoto wengine  kwa kupitia kucheza ,wakubwa kuwapa malezi yenye mwitikio   na kuona au kusikia vitu vizuri wanajifunza vitu vingi ambavyo watakuwa navyo na baadaye kuwa watoto wema”.amesema Kwesigabo.
Kwesigabo amesema watoto wasipopata malezi na makuzi bora wanakuwa kwenye hali ya viashiria hatarishi ambavyo wazazi wakiwa wanamigogoro na mtoto anaona,umasikini kutopata lishe bora,kumfungia mtoto ndani asichangamane na watoto wenzake.
Ofisa Maendeleo ya Jamii  mkoa wa Shinyanga  Bestina Gunje  akielezea kuhusu mpango mkakati wa taifa unaotokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambapo ulianza 2021 hadi 2024 /2025 ambapo  mkoa nao ulitoa baadhi ya vipengele vinavyohusu  mazingira ya mkoa wa Shinyanga kwa kuangazia mambo nane.

Gunje amesema mambo manane yaliyoainishwa kwenye  mpango mkakati wa mkoa  ni kuimarisha wananchi kiuchumi,kuondoa ukatili kwenye maeneo ya sokoni, watoto wa kike kupelekwa shuleni.

“Mafanikio yalipatikana kupunguza mimba za utotoni, maeneo ya sokoni  kumepungua vitendo vya ukatili ,utolewaji wa mikopo kwenye makundi ya wanawake,vijana na walemavu bila riba  na imani potofu zenye madhara zimepungua  na sasa wadau wote tujivunie  kwenye mafanikio haya” amesema Gunje.

Gunje amesema wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa vijana zaidi ya 5000,  kugawa taulo za kike kwa mabinti walioko shuleni  ili kuhamasisha  wasikwame masomo yao, kujenga vituo jumuishi  vya wahanga wa ukatili,kupata magari mawili na kuhuisha kamati za Mtakuwwa  za kwenye kata.

Gunje amesema mkoa  ulioana uhuishe mpango mkakati wa awamu ya pili ulioanza kufanya kazi mwaka 2025/2026 hadi 2030 ambapo katika mambo manane mojawapo kuimarisha uchumi kwenye familia kwa kuendelea kutoa mikopo kwenye makundi maalum isiyo na riba na  machinga wote wenye sifa wakope kwenye benk  na pia kuwaweka wanaume kwenye mpango huo waweze kueleza nao changamoto zao wanazofanyiwa ukatili.

Kwenye mpango huo tumeingiza mpango mpya ambao haukuwepo ambao ni  teknolojia  ya habari kukua kwa  kasi kubwa ambapo tumetaka matumizi ya teckonolojia  iliyopo iwe salama kwa watu wote hata kwa watoto kwani wazazi wamekuwa wakiwaachia simu za mkononi na runinga nakuaacha waangalie bila kufuatilia wanachoangalia.
Lucy Maganga kutoka  Shirika la Ics ambalo ni kinara wa Malezi na Makuzi ya watoto mkoa na  linalofanya uratibu  ngazi ya mkoa kwenye jamii  na jukumu lao kuu ni kuratibu wadau wote wanaotekeleza shughuli zote za malezi na makuzi  ya watoto wadogo ( ECD) kuhakikisha wanaelekea kwenye mrengo mmoja.

"Tumekuwa tukitoa   huduma ya ushauri   zinazotolewa ili  watoto  wawe na afya bora na endelevu  na wamekuwa wakifanya ushawishi kwa Halmashauri katika  kutenga  bajeti ili kuhakikisha watoto wenye  umri wa miaka 0 hadi 8 wanapewa huduma stahiki"anasema Maganga.




 

Post a Comment

0 Comments