MLINDE MTOTO KWA CHANJO YA POLIO



Na  Kareny  Masasy, Shinyanga

WATOTO wenye umri wa kuanzia miaka sifuri  hadi kumi  mkoani Shinyanga wanatarajiwa kupatiwa chanjo  ya Polio ili kuwazuia kupata virus vya ugonjwa huo  nakuweza kuwaepusha na ulemavu wa kudumu au vifo.

Hayo yamesemwa leo na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Dk Yudas Ndungile  alipokuwa akifungua kikao  na waandishi wa habari huku akieleza Kampeni ya Uzinduzi wa  kutoa chanjo ya Polio itakayoanza rasmi tarehe 24 hadi tarehe 27 mwaka 2026   kupitia vituo vya afya, nyumba kwa nyumba,vituo vya kulelea watoto mchana (Daycare)pamoja na shuleni.

“Wazazi watatakiwa kuwapeleka watoto  hao ambao ni walengwa kwani mkoa huu unatarajia kuwafikia watoto takribani  781186 ambapo utafiti uliofanyika jijini Mwanza  umeonyesha maji taka yanavimelea vya Virus vya polio  na serikali ikaona kuwapatia chanjo watoto hao  ili kuweza kuwanusuru na ulemavu wa kudumu au vifo”amesema Dk Ndungile.

 Dk Ndungile amesema  kampeni hiyo itafanyika kwenye mikoa ya kanda ya ziwa  ambayo ipo kwenye hatari ya vimelea kusambaa  nakuwa hatari kwa watoto na serikali  kuona ni vyema kuanza kuzuia kwa kuwapatia chanjo mapema  kuweza kuzuia kabla ya kupatikana kwa madhara makubwa.

“Takwimu hizi zimechakatwa na NBS  kwa kushirikiana na Wizara ya Afya  kulingana na  maeneo husika ambapo kila Halmashauri zitatoa chanjo ya polio kwa watoto hao ikiwa  Halmashauri ya Ushetu watoto 148,557, Kahama Manispaa   145,820,Msalala 138,172,Kishapu 120,130, Halmashauri ya Shinyanga  166,428 na Manispaa ya Shinyanga 62,192”amesema Dk Ndungile.

Mratibu  Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Shinyanga  Moses Mwita alisema  ugonjwa wa polio  umekuwa tishio kwa miaka mingi ambapo nchini Tanzania  kwa mara ya mwisho mtu aliyegundulika na ugonjwa huyo  ni mwaka 1996  hivyo  serikali imekuwa ikitoa chanjo hii kwa watoto wenye umri tofauti tofauti baada ya kuzaliwa.

Mwita amesema chanjo ya polia  baada ya kampeni kuanza mwezi huu itatolewa kwa njia ya matone siyo Sindano na watapita wataalamu kwenye kila nyumba kuanza kuhamasisha  lengo watoto waliokusudiwa wapate chanjo hiyo ni  bure na haina madhara yoyote.

“Chanjo hiyo imelengwa kwa mikoa saba ambayo ni Mwanza,Singida,Mara,Tabora Simiyu,Geita na Shinyanga  baada ya Kuzindua ngazi ya mkoa kila Halmashauri nazo zitafanya zoezi hilo  nakuwafikia watoto walilengwa na tayari wataalam wamepatiwa maelekezo zaidi amesema Mwita.

 Mtoa Elimu kwa Umma  Idara ya kinga kutoka wizara ya Afya Anne Shuma  amesema waandishi wa habari wanategemewa kuhamasisha na kufikisha ujumbe kwa wananchi  ambapo hakuna mgonjwa wa polio wala mlipuko wa polio lakini kuna vimelea na sasa serikali imeanza kuchukua tahadhari kuwawekea kinga hata kama alikwisha chanjwa atarudia tena.

“Watoto hawa wengi watakuwa shuleni na nyumbani na chanjo hizi zitatolewa bure serikali imegharamikia ndiyo maana haziuzwi maeneo yoyote hivyo wazazi wajitokeze kuwalinda watoto na zoezi litazinduliwa kwenye mikoa hiyo kitaifa litazinduliwa mkoani Mwanza na Waziri wa Afya”amesema Shuma .

 



Post a Comment

0 Comments