WATU 63 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI WAKUTWA NA VIELELEZO


Na Kareny  Masasy,

Shinyanga

JESHI la polisi Mkoani Shinyanga limewashikilia  watu 63 wakiwa na vielelezo mbalimbali ikiwemo kielelezo cha mafuta ya dizeli lita 295 na pikipiki 14.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa hapa  Janeth Magomi amewaeleza  waandishi wa habari  leo  kuwa katika oparesheni mbalimbali zilizofanyika kwa  kuanzia   mwezi April mwaka huu  ilikuwa na lengo la  kubaini na kuzuia  uhalifu.

Kamanda Magomi amesema  msako mkali ulifanyika na  wameweza kuwashikilia  watuhumiwa 63  wakiwa na makosa mbalimbali ambapo vielelezo walivyokamatwa mojawapo ni lita 295 za mafuta ya dizeli na pikipiki 14.

 Kamanda  Magomi amesema  vitu vingine walivyo kamata ni  noti bandia zenye thamani ya shilingi   81,000,simu za mkononi 98 na betri za simu 86.

Kamanda  amesema  wamefanikiwa kukamata pia vipande 21 vya chuma ,Redio nane,viti vya  plasitiki sita,mifuko 13 ya mawe yadhaniwayo kuwa na madini, Spika tano,mashine ya kuoka mikate moja na mbuzi saba .

Wakati huo huo Kamanda amesema  miongoni mwa watu 63  waliokamatwa wapo waliokuwa wanajihusisha na madawa ya kulevya ambapo  walikamata Mirungi  kilogramu  103,bangi kilogramu  1,100.

“Yapo mafanikio ya kesi  saba zilizokuwa zimepelekwa mahakamani   ambapo kesi tano za wizi washtakiwa  saba wamehukumiwa  kifungo  cha  kwenda jela miezi sita  na wengine miaka minne  na kesi moja  kutishia kuua kwa maneno na kesi moja shambulio la kudhuru mwili na kuhalibu mali”amesema Kamanda Magomi.

Kamanda Magomi amesema  tayari wamefanya mikutano 182  ya uelimishaji katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo shuleni na vjiwe vya waendesha bodaboda  ili jamii ielewe umuhimu  wa kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa na ulinzi na usalama.


Post a Comment

0 Comments