MWANAFUNZI AJINYONGA KWA KUTUMIA MKANDA WA SKETI YAKE

MWANAFUNZI wa kidato cha nne Rebeka  Maganga (17) anayesoma Shule ya Sekondari Old Shinyanga amedaiwa  kufariki  dunia kwa kujinyonga ndani ya chumba alichokuwa akilala  nyumbani kwao alikokuwa akiishi na  babu yake Mshala Peter (56).

Mwanafunzi huyo alijinyonga  kwa kutumia mkanda wa sketi yake  kisa kikidaiwa  kukosekana shuleni wiki mbili bila taarifa  nakutakiwa na walimu kwenda kumuita mzazi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi amethibitisha  kutokea kwa tukio hilo juzi   majira ya saa saba mchana katika eneo la kata ya  Old Shinyanga  ambapo mwanafunzi huyo alikuwa akiishi.

 Kamanda Magomi amesema  uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu alitumia mkanda wa sketi ya shule kujinyonga na kisa chake ni kukosekana shuleni kwa muda wa wiki mbili nakutakiwa na walimu akamuite mzazi.

 “ Tunavyoona  tukio la mwanafunzi kujinyonga limetokana nikuwa na msongo wa mawazo baada ya kurudishwa nyumbani na walimu  kufuatia kutohudhuria masomo kwa muda wa wiki mbili bila taarifa”amesema  Kamanda Magomi.

Kamanda Magomi amesema malezi ni jambo la msingi wanasikitika kuona   mtoto huyo kulelewa na babu pekee huku wakishauri  wazazi  kutowatelekeza watoto  hivyo aliwapongeza walimu kuwa na ushirikiano na mlezi huyo.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Senyenge Kijiji cha Old Shinyanga Benjamin Andrew amesema  walipokea taarifa za tukio hilo majira ya saa sita mchana na kufika eneo la tukio ambapo walimkuta mwanafunzi huyo  ananing’inia  amefariki.

Andrew amesema   mwanafunzi huyo alikosekana  shuleni kwa muda wa wiki mbili na walimu walimtaka arudi nyumbani akamuite mzazi  ambapo alikuwa akiishi  na babu yake .

 

Post a Comment

0 Comments