MBUNGE VITI MAALUM SHINYANGA MWANAHAMIS ATAKA SHULE YA MSINGI NYABUSALU USHETU IWE MAALUM



MBUNGE  viti Maalum  Mkoani Shinyanga Mwanahamis   Mukunda  ameomba shule ya msingi Nyabusalu iliyopo kata ya Bulungwa halmashauri ya Ushetu iwe shule  maalum  na walimu wajengewe nyumba za kuishi.

Walimu hao wamekuwa wakifanya kazi kubwa kwenye  shule hiyo nakuifanya  kushika nafasi ya nne kitaifa  kwa matokeo ya  darasa la saba mwaka huu na mwaka jana ilifanya vizuri  pia.

Hayo yamesemwa  na   Mbunge huyo mbele ya Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Nyamilangano  Halmashauri hiyo.

“Ninachoomba walimu wa shule hiyo wako nane  na  jumla  ya  wanafunzi  ni 438  na changamoto iliyopo miundombinu ya shule siyo mizuri na hakuna nyumba za  walimu  kwani wanaishi  mbali na shule”amesema Mukunda.
Mbunge wa jimbo hilo Emmanuel Cherehani amesema  mwaka jana  walimu hao walipofanya vizuri aliwaita bungeni nakuwapongeza huku  mashine ya kuprint  na kompyuta kama zawadi na kuniahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi.

 Kweli walimu hawa hawaja niangusha hata  mwaka jana tulikwenda kuitembelea shule hiyo tukiwa na mkuu wa mkoa Mboni Mhita kwa lengo la  kuwapongeza wazazi   na walimu na kuwapa kombe la ushindi  na  fedha shilingi Milioni 1.5".amesema Cherehani 

Hata hivyo shule hiyo matokeo ya darasa la nne mwaka 2025 ilishika nafasi ya kwanza kitaifa  na matokeo ya  darasa la saba mwaka huu imeshika nafasi ya nne kitaifa.



Post a Comment

0 Comments