MADIWANI USHETU WAISHAURI BODI YA TUMBAKU NA USHIRIKA WAELEZA WALICHO JIFUNZA KATAVI

BAADHI ya madiwani  wa  Halmashauri ya Ushetu  wilayani Kahama Mkoani Shinyanga  wameshauri  chama kikuu cha Ushirika wilayani humo (Kacu) na bodi ya tumbaku kushirikiana  kwa pamoja  kusimamia makampuni yanayonunua zao la   tumbaku kwa wakulima  sababu ni moja ya chanzo cha mapato ndani ya halmshauri.

Hayo  yamesemwa  leo kwenye kikao cha baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 kuanzia mwezi Julai  hadi  Septemba  huku  wakisitiza  kutumia mbinu  ya halmashauri  ya mkoa wa Katavi kwa wilaya ya Mpanda na Tanganyika walikokwenda kujifunza namna ya utunzaji wa  Misitu  kwa kutumia hewa ya ukaa na  ukusanyaji mapato  ya ndani.

Diwani wa kata ya Bukomela   Kulwa Shoto amesema   mnamo mwezi Oktoba mwaka huu walikwenda ziara   mkoani Katavi  walifanikisha kuona ukusanyaji wa mapato kwenye zao la tumbaku  nakuona  chanzo cha hewa ya ukaa  kinachotunza pia misitu  sanjari na utunzaji wa mazingira

Diwani  Shoto amesema   wakulima wafundishwe  kama walivyoona mkoani Katavi  huku Ushetu asilimia kubwa  wamebaki kukopa  nakutorosha zao la tumbaku  na baadhi ya makampuni ya ununuzi zao hilo yamekuwa sio maadilifu  na bado yanadaiwa na halmashauri  .

    “Sasa ifike mahali tuone  kuwa na  vyama vyenye tija  kuliko kuwa na vyama vingi vya msingi  visivyokuwa na  tija na kutoingiza mapato kwenye halmashauri yetu hili tunashauri  bodi ya tumbaku na chama kikuu cha Ushirika wasimamie vyema ”amesema diwani Shoto

wenyekiti wa Halmashauri hiyo Gagi Lala  amesema   ifike wakati vyama vya msingi  vishirikiane na   wakulima kuondoa changamoto zilizopo   na mapato yalipwe ipasavyo .
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Hadija Kabojela amesema  baada ya kutoka kwenye ziara hiyo  hatua ya kwanza  walifanya mchakato  wa awali  kuanzia kwenye misitu  na pale panapostahili  kuweka  bajeti   waweke  na kushauri  bodi ya tumbaku  wasimamie  makampuni ili halmashauri iweze kupata mapato yake.

Ofisa Mipango wa Halmashauri hiyo Shigela  Ganja  akisoma taarifa  ya utekelezaji wa miradi  ya robo ya kwanza ya mwaka  wa fedha 2026/2027  ambapo alisema wamepokea shilingi  bilioni  2.9 ni fedha za ruzuku kutoka serikali kuu   pamoja na  makusanyo ya  mapato ya ndani ya halmashauri.

“Katika ruzuku ya serikali  kuu wamepokea fedha zote za  utekelezaji wa mradi  miwili   zilizotengwa  ambayo ni  ujenzi wa jengo la utawala   na mradi wa maghala  ambapo ukusanyaji wa mapato ya ndani wamekusanya kiasi na kutoa  shilingi Milioni 172 zimepelekwa kwenye utekelezaji wa miradi  ya Maendeleo”amesema  Shigela.


 

 

Post a Comment

0 Comments