MBUNGE JIMBO LA KISHAPU ATOA KILIO KUKOSA HUDUMA YA MAJI KATA SABA

Naibu waziri wa Maji  Mhandisi Kundi  Mathew ametoa  matumaini kwa wakazi wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga kuwa  wizara ya maji  imekuja na habari njema kuwa maeneo  ya kata ya Ngofila na Sekebugoro ikiwemo vijiji saba  yamefanyiwa usanifu wa kina ili yaweze kupata maji nakutengewa gharama ya shilingi bilioni 5.7 kutekeleza.


  Naibu waziri Mathew amesema hayo  baada ya mbunge wa jimbo la Kishapu Lucy Mayenga kueleza mbele ya waziri mkuu Mwigulu Nchemba  kuwa  kata saba kati ya kata 29 zilizopo hazina maji safi na salama wala chanzo wanachokitegemea kupata huduma ya maji.

iNaibu waziri Mathew amesema jimbo la Kishapu lina vijiji 117 na vijiji 41 pekee ndiyo havina maji safi na salama  na katika miaka mitano ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwa madarakani  miradi 16 yenye thamani  ya shilingi bilioni 19 imekamilika.

"Hapa Kishapu kulikuwa na miradi  sita yenye thamani ya shilingi bilioni 5.9 na imekamilika na itahudumia vijiji kumi  na nchi nzima kuna vijiji 12,333 na kati ya hivyo vijiji 1575 havina maji ikiwemo Jimbo la kishapu vijiji 41"amesema  Mathew.
Naibu Waziri Mathew amesema   kuna  kata mbili za Ngofila na sekebugoro  na vijiji saba ambapo tayari maeneo hayo yamefanyiwa usanifu  wa kina kwaajili ya kupata maji  na gharama yake imetengwa shilingi bilioni 5.7 kwenda kutekeleza.

Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amewaeleza wananchi wa jimbo la Kishapu kuwa miradi mingi ilikwama kutekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo kwa sasa fedha zinaelekezwa kwenye wizara husika ili miradi iliyopangwa kutekelezwa

Mbunge Lucy Mayenga amesema  ametoa kilio cha wananchi wake kuhusu kata saba kati ya 29 kukosa kabisa  mtandao wa maji safi na salama huku akitaka kujua lini wananchi watapata maji?.

mwisho.

Post a Comment

0 Comments