WAKULIMA wameshauriwa kutumia wataalamu na mbegu zilizo bora za kuua magugu kupandia,kunenepesha mmea na
baada ya mavuno kuweka katika kifungashio salama.
kwani wakulima wamekuwa wakipata mazao machache au kukosa kabisa nakutumia gharama nyingi kwa kutofuata ushauri wakati wa kilimo na kusababishia hasara.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Seedco Kahade Dada wakati wa uzinduzi wa duka la Wakala wa Pembejeo za Kilimo Mjini Kahama Yohana Agribussines nakueleza baadhi ya wasambazaji wa Mbegu hizo wamekuwa wakiwauzia wakulima Mbegu ambazo hazifai kwa matumnizi ya Kilimo.
Mkurugenzi wa Wakala Mkuu wa Pembejeo za kilimo ya Agri- Buisness Company Limited Yohana Magadula amesema kuwa ameamua kufungua duka hilo kwa lengo la kushirikina na wafanyabiashara wenzake wa Pembejeo za kilimo kwa lengo la kumsaidia Mkulima kuondokanana umasikini.
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo kutoka katika Halmashauri Manispaa ya Kahama Liberia Sabini ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo amesema wanamshukuru wakala huyo kuanzisha duka katika Manispaa ya Kahama kwani kwa sasa sekta hiyo imekuwa imesambaa katika maeneo mbalimbali.
Akiongea kwa niaba ya Wakulima Joseph Simon kutoka Halmashauri ya Ushetu alisema kuwa awali walikuwqa wakifuata mbegu za Seedco Mkoani Tabora na kuongeza kuwa wakulima wafuate kilimo cha kisasa ili wapate mazao mengi.







0 Comments