MBUNGE wa jimbo la Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga Emmanuel Cherehani ameomba kujengewa kituo cha afya kata ya chona ikiwa wananchi wake wanateseka kwa kukosa huduma kwenye eneo hilo.
Mbunge cherehani amesema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Nyamilangano mbele ya Waziri mkuu Mwigulu Nchemba huku akipongeza serikali kumpatia jimbo lake shilingi Milioni 657 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya Ulowa na shilingi Milioni 600 za ujenzi wa kituo cha afya Idahina.
"Nina shukuru sana jimbo la ushetu kupatiwa zaidi ya shilingi bilioni mbili za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo bado changamoto moja kubwa ni kukosekana mradi wa kimkakati hata mmoja kama maeneo mengine ninaomba ujenzi wa barabara hii yenye kilomita 54 kutoka Kahama mjini hadi Jimbo la Ushetu*amesema cherehani.
Mbunge wa vitimaalum mkoani Shinyanga Mwanahamisi Mukunda amesema Halmashauri ya ushetu ina vituo vya afya vitano kati ya kata 20 zilizopo ila kata ya chona haina kituo cha afya kina mama wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amesema yeye anatoka kwenye kata hiyo amesema kweli haina kituo cha afya aliomba kijengwe kwani wapo tayari kutoa maeneo .
"kuhusu ujenzi wa barabara hilo mtuangalie sana waziri mkuu na kweli kijiji chetu cha chona au kata haina kituo cha afya na eneo nipo tayari kutoa"amesema Mlolwa.
Naibu Waziri ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa (tamisemi) dk Festo Dugange amesema hapa nchini kuna hospitali 183 na hospitali 12 zilizo ngazi ya wilaya na Zahanati ni 2700 hivyo jitihada zinaendelea kuongeza vituo vya afya nchi.
Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amesema utekelezaji wa miradi utaendelea na ujenzi wa kituo cha afya wanaiachia halmashauri na mbunge kuhakikisha kituo cha afya kinajengwa kata ya chona.
Baadhi ya wananchi wa jimbo la Ushetu Onesmo Kulwa na Gaudensi Rutazika walifurahi baada ya kusikia miradi mbalimbali itatekelezwa ikiwemo barabara na ujenzi wa kituo cha afya chona.
mwisho.








0 Comments