Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga dk Honoratha Rutatinisibwa amesema hayo kwenye kikao cha utelelezaji wa programu hiyo katika kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi April hadi Septemba mwaka 2026 huku akieleza waandishi wa habari ni muhimu sana kwani wamekuwa wakiibua penye changamoto na serikali kutekeleza nakutoa elimu.
Dkt Rutatinisibwa amesema ulimwenguni kuna takribani watoto Milioni 250 wenye umri chini ya miaka mitano ambao wanapatikana kwenye nchi zenye uchumi wa chini na uchumi wa kati ambao wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua zao za ukuahi.
"Takribani robo tatu sawa na asilimia 66 ya watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano waliokusini mwa jangwa la sahara wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua timilifu ya ukuaji wao kutokana na kukosa malezi bora,umasikini ,utapiamlo na matatizo mengine"amesema dkt Rutatinisibwa.
Amesisitiza "Ninawaombeni wataalamu wenzangu kwenye halmashauri zote sita mtoe ushirikiano mnapohitajika kwenye vipindi mbalimbali vya redio katika programu hii ni muhimu kwani jamii ikielewa vizuri itakuwa makini katika suala la malezi na Makuzi nakufikia hatua nzuri ya ukuaji timilifu".
Dk Rutatinisibwa amewashauri wajawazito wahudhurie kliniki kwa hatua zilizopangwa ili wataalamu waone maendeleo ya mtoto na makuzi yake ya awali nakuwaepusha na vifo au ulemavu unaozuilika kama kichwa kikubwa na mgongo wazi
Mratibu wa PJT-MMMAM mkoa wa Shinyanga Lyidia Kwesigabo ambaye pia ni Afisa Ustawi wa Jamii mkoa amesema waratibu kwenye halmashauri wajitahidi kutekeleza kwa maazimio waliyokubaliana nakuhakikisha kadi ya ECD (scorecard ECD) inajazwa kwa kufikia malengo pale penye mapungufu paangaliwe nakuwekwa sawa.
Kwesigabo amewakumbusha waratibu hao kuhakikisha maeneo yanayojengwa kama masoko na maeneo mengine muhimu kuwekwa vituo vya malezi vya kijamii (ECD Corners) kwani itasaidi watoto kupata malezi yenye mwitikio ikiwemo ulinzi na usalama.
Ambapo kila Halmashauri iliwasilisha taarifa ya utekelezaji kwenye maeneo yao huku wakieleza mafanikio ya upatikanaji wa chakula shuleni,upatikanaji wa chanjo kwa watoto na wajawazito ikiwemo vyeti vya kuzaliwa kwa watoto.
Mwakilishi kutoka shirika la Invest Children in Society (ICS) Lucy Maganga amesema wamekuwa wakiratibu shuguli zote za programu hiyo huku akipongeza serikali ya mkoa wa shinyanga na vyombo vya habari kutekeleza kwa kutoa elimu huku akishauri elimu kwenye jamii iendelee kutolewa zaidi hata kama programu inakwisha kwani bado upo umuhimu kwenye nguzo tano ambazo zimekuwa zikisisitizwa.








0 Comments