KATIBU mkuu wizara ya Madini mhandisi Yahya Samamba ametoa magizo kwa wamiliki na mameneja wa migodi nchini kuhakikisha wanaboresha maeneo ya uchimbaji wa madini hasa upande wa maduara, uwekaji wa matimba na vyoo ili kuwe salama kabla ya mvua za El-Nino zinazotabiliwa na Mamlaka ya hali ya hewa (TMA) nchini kuanza.
Hayo yamesemwa leo na Mhandisi Samamba alipokuwa mgeni rasmi katika semina ya wachimbaji wadogo kwaajili ya maamdalizi ya kukabiliana na athari zamvua za El-Nino katika maeneo yote ya wachimbaji wadogo ambapo Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo ianze kuchukuliwa tahadhari ya kuangalia miundombinu.
Mhandisi Samamba amesema asilimia 70 ya ajali zote mgodini zinatokana na udongo kulowana nakuwa mzito ,matimba yanakuwa ya muda mrefu yanakuwa tayari yameoza, hivyo jitihada zinatakiwa zianze kufanyika mapema kabla ili athari za watu kufa zisitokee .
"Mojawapo ya majanga yanayo sababisha vifo vya watu wengi ni ajali za mgodini lakini tukijitahidi kutengeneza miundombinu mizuri mfano kuweka mifereji itakayotiririsha maji, kubadilisha matimba nakuweka yenye ubora na vyoo vizuri kuepuka pia ugonjwa wa kipindupindu" amesema mhandisi Samamba.
Mhandisi Samamba amesema maazimio yapatikane mwisho wa kikao yakuwekana sawa katika utendaji kazi kwa ushirikiano kutoka kwa maafisa madini mikoa ikiwemo kutoa ushauri kwa lugha za kitaalamu.
Mwakilishi wa shirikisho la vyama vya wachimbaji nchini (Femata) ambaye ni katibu wa chama cha Madini mkoa wa Shinyanga (Shirema) Gregory Kagusi amesema upo umuhimu wa mafunzo haya ambayo wanakwenda kujari athari za mvua ziinazotarajiwa kunyesha hivyo watakwenda kuhakikisha wanajilinda kama inavyoelekezwa.
Mwenyekiti wa Chama cha wakaguzi wa migodi nchini (Chawumita) Shija Musa amesema wamekwisha anza ufungaji wa matimba na kufukia mashimo ambayo hayatumiki nakuhakilisha yale yote yanayoelezwa na serikali wanayatekeleza.




0 Comments