WAFANYABIASHARA wa soko la Namanga CDT Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wamehimizwa kufanya usafi kila wakati ili kuweka soko safi na kuzibua mifereji inayotuama maji.
Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya mjini Kahama Godson Andrew alikuwa akihamasisha usafi kwa wafanyabiashara wa soko hilo huku akieleza changamoto iliyopo ni baadhi ya wafanyabiashara wa maduka kutofanya usafi.
Andrew amesema zoezi la kufanya usafi liwe la kila jumamosi kabla ya kuanza biashara usafi kwanza ufanyike ili soko na maeneo ya stendi yawe safi.
Mwenyekiti wa soko hilo amesema walilaa kikao na kuweka mikakati ya namna ya kuweka mazingira safi na atakaye kaidi hatua zitachukuliwa.
baadhi ya wafanyabiadhara wa soko hilo Christina Mbelwa amesema suala la kufanya usafi nila muhimu kwao sababu wanapokea wateja wengi na kuuza vyakula.
tutasimamia suala la usafi kila mmoja hili. tumelipokea ila ushauri tunaomba mitaro iwekwe vizuri maji machafu yamekuwa yakitiririka.





0 Comments