DIWANI AANZA KUFUFUA BARABARA YA LUMUMBA B MTAA WA IGALILIMI


BARABARA  ya Lumumba B yenye urefu wa kilomita moja  iliyopo mtaa wa Igalilimi  mlimani Kata ya Kahama mjini  Manispaa ya Kahama  imeanza zoezi ya kufunguliwa na kutarajiwa kukarabatiwa ili iweze kuunganisha  mitaa mingine  kupitika  kwa urahisi.

Barabara hii niya miaka mingi inaanzia kata ya Nyahanga nakupita pembeni mwa jengo la kituo ch polisi  nakuunganisha mitaa mingine.

Diwani wa kata ya Kahama mjini  Godson Andrew amesema hayo leo alipotembelea eneo la barabara hiyo yenye urefu wa kilomita moja iliyokuwa haipitiki kwa waenda kwa miguu na vyombo vya moto kutokana na kuwa  na  miamba ya mawe  yaliyokuwa kizuizi kikubwa.

Andrew amesema kupitia Halmashauri walianzimia kutenga shilingi Milioni 300 kwaajili ya kufungua barabara ambazo zilikuwa hazipitiki kirahisi hivyo hapa mjini wameamua kufungua barabara ya Lumumba B eneo la mtaa wa Igalilimi.

Andrew amesema wamefungu barabara hii yenye urefu wa kilomita moja ilikuwa haipitiki kirahisi  imeanza kuondolewa mawe na  sasa ni kipindi cha miezi miwili kuanza kutoa mawe hayo na kuyahifadhi baadaye kuja kufanya kazi nyingine.

“Kipindi hiki cha mvua tunaangalia sana barabara ziweze kupitika  na barabara hii ni muhimu sana kwani ipo katikati ya mji natumaini wafanyabiashara watajitokeza kumulika fursa  utakuwa ni eneo la kibiashara zaidi”amesema Andrew.

Andrew amesema changamoto ya kuvunja mawe ndiyo inachelewesha wanatumia njia ya kawaida taratibu sana ingewezekana kutumia vifaa vya kisasa  ili kurahisisha kuikarabati na kufunguliwa ..

Thobias Mtabingwa  amesema  barabara hii ilikuwa na changamoto kubwa ya kutopitika hivyo anaipongeza serikali kuiona nakuanza kuifanyia kazi kwani  itawarahisishia  kupita na kwenda maeneo mbalimbali kwa urahisi.

Onesmo Musa dereva bodaboda amesema barabara hii  ipo miaka mingi ilikuwa haipitiki  kirahisi  na ilikuwa inatisha marekebisho yameanza unafuu wa kupita umeanza kuonekana  na imerahisisha kuunganisha mitaa na kata.


Post a Comment

0 Comments