DIWANI wa kata ya Kahama mjini Mnispaa ya Kahama mkoani Shinyanga Godson Andrew amewashauri wauzaji wa matunda kutii agizo la serikali kwani biashara zote ziko sawa na zinathaminiwa kwani ni vyanzo vya mapato kwenye halmashauri na familia zao.
Andrew amesema hayo leo kwenye zoezi la kuhamasisha usafi kwenye maeneo mbalimbali ya kata hiyo ikiwemo eneo la soko la Namanga CDT huku akieleza wafanyabishara wanapaswa kujisimamia kwani watumishi wa halmashauri wakipita ni kwenda kuwakumbusha tu wajibu wao.
Andrew amesema Manispaa haijakataa mfanyabiashara wa matunda asifanye biashara na kila biashara ina umuhimu wake hakuna aliyedharau biashara ya mtu kinachotakiwa ni kwenda kwenye maeneo yaliyo rasmi nakuondoka kuuzia kandokando ya mitaro ni hatari .
“Kujitambua kwako ndiyo serikali yenyewe hivyo wafanyabiashara wa matunda nendeni kwenye maeneo mliyopangwa ikiwezekana mnaweza kuuza mkiwa mmepanga kwenye vibanda hilo halikataliwi”amesema Andrew.
Andrew amesema wananchi wa kata ya mjini wasisikilize maneno ya mitaani kuwa stend ya CDT itahama hapana itaendelea kuwepo na ile inayojengwa itakuwepo itakuwa ni mgawanyiko tu wa maeneo na kuongeza vyanzo vya mapato ili halmashauri ipate fedha.
“ Mji huu wa kahama umekuwa mkubwa na sisi wenyewe tujisimamie tusisubiri kusukumwa wafanyabiashara tuwe kama watu wa bodaboda wamejiwekea utaratibu wao na mnapopanga biashara kandokando ya mitaro ni hatari kwani tumeambiwa mvua zitanyesha juu ya wastani na tunaangalia mitaro isikwame maji iwe safi muda wote”amesema Andrew.
Andrew amesema lipo eneo lililotengwa kwaajili ya kuuza matunda hivyo siku ya kugawiwa maeneo wawahi kushika nafasi mapema na hatuja ruhusu mfanyabishara asiuze matunda ndani ya chumba bali kandokando ya mitaro tu na maeneo yasiyo rasmi na maelekezo yametolewa.
Andrew amewashauri Wafanyabiashara kuwa wamoja wapo wataalamu wa mipango miji kama wamepata eneo wajitahidi kushirikisha uongozi wa mtaa au kata ili kuweza kuona namna ya eneo hilo kurasimishwa kama halina changamoto yoyote na wao kufanya biashara.
Baadhi ya wafanyabiashara wa matunda kata ya mjini wamedai kupewa maeneo ambayo hayana biashara na wanapoondolewa bidhaa zinavurugika kwani wamekopa fedha nakudaiwa marejesho na familia inatakiwa kupata chakula.


0 Comments