RAIS SAMIA APONGEZWA KUWEKA KIPAUMBELE WAWEKEZAJI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan , amepongezwa na kupewa shukrani kwa kutoa fursa kwa Wawekezaji wa ndani kuwekeza na kupatikana kwa ajira kwa VIJANA.

Hayo yalielezwa na Meneja wa Kituo Cha MAFUTA Cha Ngara Oil, kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Nuru Christopher Nzoya, mbele ya mkimbiza Mwenge Kitaifa, Michael Mwang'onda.

Nzoya akiongea kwa niaba ya mmiliki wa Kituo Cha MAFUTA hicho, alisema fursa ya uwekezaji huo utasaidia kutoa ajira kwa VIJANA wengi AMBAO hawana ajira na kuwawezesha kujikimu kimaisha.

Aidha alisema uwekezaji huo ambao licha ya kusaidia ajira na vijana kujikimu kimaisha pia utachangia kukuza uchumi wa Taifa.

Alisema mradi wa ujenzi huo ulioanza Januari 7, mwaka huu unatarajia kukamilika Oktoba 30, mwaka huu Ikiwa na lengo la kutekeleza sera za nchi inayoshirikisha wadau wa ndani katika uwekezaji sekta mbalimbali za kibiashara kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi na kutoa fursa za ajira kwa Watanzania.

Alibainisha kuwa Kituo hicho kitapokamilika na kuanza kutoa Huduma ya mafuta katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, kinatarajia kutoa ajira kwa watumishi 20. Na kwamba mradi huo Hadi kukamilika utagharimu kiasi Cha Shilingi 821,500,000/-.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang'onda, baada ya kutembelea Kituo hicho na kujiridhisha kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Kituo hicho,  alipongeza kwa mwekezaji Mzawa kuwekeza mradi mkubwa AMBAO utaleta tija katika eneo husika.

Mwang'onda alitoa ushauri kwa Halmashauri zote nchini kuweka mazingira mazuri ya miundo mbinu ili kuwezesha Wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kumudu kuwekeza ili kujenga uchumi imara wa taifa.

Alisema kuweka miundo mbinu rafiki kwa Wawekezaji ni kutekeleza Sera ya Nchi ya kushirikisha Wadau wa ndani na nje kuwekeza katika sekta mbalimbali za kibiashara hatua itakayosaidia kukuza uchumi wa Taifa,kujikimu kimaisha na kutoa  ajira kwa vijana.

Post a Comment

0 Comments