KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Wazo Mwang’onda ameweka jiwe la msingi kwenye kituo cha afya kilichopo kijiji cha Bugera kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyangakwa mujibu wa taarifa iliyotolewa imeeleza kituo kimejengwa kwa fedha za serikali kwa kuletwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zimetolewa shilingi MIlioni 250 na awamu ya pili zimetolewa shilingi Milion 657.
Kiongozi wa Mbio hizo Mwang’onda amesema yuko tayari kuweka jiwe la msingi kwenye kituo hicho ambacho kinajengwa kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi karibu kupata matibabu
“Nimejionea leo jengo la wagonjwa wa nje (OPD) limekamilika bado jengo la mama na mtoto pamoja na jengo la upasuaji yanaendelea kujengwa hivyo miundombinu hii ikikamilika itunzwe vizuri”mesema Mwang’onda.
Akiendeleza kutoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru Mwang’ando amesisitiza suala la amani na utulivu ndani ya nchi liendelee kuwepo kwani ndiyo tunu iliyobaki kwa watanzania wote na mwenge huu wa Uhuru uliasisiwa na Hayati baba wa Taifa Julius Nyerere hilo nila kujivunia kwa siku zote.
Mbunge wa jimbo hilo Emanuel Cherehani amesema maendeleo yameanza kwa hatua baada ya kupata eneo hilo lililokuwa linamilikiwa na chama cha Mapinduzi( CCM) kwa kupewa ekari kumi kujenga kituo ili wananchi wasiteseke kutembea umbali mrefu kutafuta matibabu.


0 Comments