KIKUNDI CHA UFUGAJI NYUKI CHAFURAHIA UFADHILI WA BARRICK BULYANHULU


Na Kareny Masasy, Msalala

KIKUNDI cha  Ufugaji nyuki Twikondele kilichopo kijiji cha Buyange kata ya  Halmashauri ya Msalala  kimefanikiwa kuwa na mizinga ya nyuki ya kisasa   117 baada ya kupewa ufadhili na Kampuni ya Mgodi ya Barrick Bulyanhulu nakuonyesha kufanya vizuri.

Katibu wa kikundi hicho Daniel Nkwande  amesema hayo  leo mbele ya kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru  Kitaifa Wazo Mwang'onda alipofika kwenye eneo la mradi wa nyuki na kitalu cha miti ya matunda kilichotumia gharama ya shilingi Milioni 25.

Nkwande  amesema wamepatiwa ufadhili na kampuni hiyo nakupewa mafunzo sanjari  na kupelekwa kwenye maonyesho ya mbalimbali ya biashara nakujifunza upatikanaji wa masoko ikiwemo kupanda miti ya  matunda kama sehemu ya uhifadhi mazingira.

"Kabla ya kufikia hatua ya kuwa na mizinga 117 walianza ufugaji mwaka 2015 wakiwa na mizinga saba ya kawaida  waliokuwa wakiifuga kwenye kikundi chao"amesema Nkwande.

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya mgodi wa  Barrick Bulyanhulu  Zuwena Semkondo amesema  awali  kikundi hicho waliwafadhili mizinga saba kama majaribio baada ya kuona wanafanya vizuri wakawapatia mizinga 110 ya kisasa.

Semkondo  amesema wameendelea kufanya kazi na jamii inayowazunguka  ambapo waliwawezesha na kuwapatia mafunzo na kuwasafirisha kwenda kwenye maknyesho ya biashara kwaajili ya kujifunza  na ufugaji umewapa manufaa wameweza kujenga nyumba za kisasa,kusomesha watoro na shughuli zingine za maendeleo.


Hata hivyo kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Wazo Mwang'onda amesema mradi wa utunzaji mazingira na upandaji miti vitalu vya miti ya  matunda ni  mzuri hivyo anawaomba waendelee kutunza na kuhifadhi mazingira kwani Rais Samia Suluhu ni kinara wa utunzaji mazingira na utumiaji wa nishati safi ya kipikia.

"Ninawapongeza kikundi hiki kwa uhifadhi na kuotesha vitalu vya miti ya matunda  kila mmoja awe rafiki wa kuhifadhi mazingira "amesema Mwang'o da.

Post a Comment

0 Comments