KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Wazo Mwang'onda ameweka jiwe la msingi kwenye jengo la wodi ya wazazi na upasuaji katika kituo cha Afya Kakola kata ya Bulyanhulu Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kilichogharimu zaidi ya shilingi Milioni 269.
Kabla ya kuweka jiwe hilo Mganga mfawidhi wa kituo hicho dkt Emanuel Boniface akisoma taarifa ya ujenzi huo leo amesema ujenzi ulianza rasmi mwezi Oktoba mwaka 2025 na kukamilika mwaka 2026 mwezi Julai.
"Serikali kuu ilileta shilingi Milioni 250 na Halmashauri ya Msalala imetoa zaidi ya shilingi Milioni 19 kwa kuboresha miundombinu ya kituo hicho"amesema Dkt Boniface.
Mbunge wa jimbo la Msalala Mabula Magangila amesema kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kata ya kakola ina takribani wakazi 51,000 lakini walikuwa hawana kituo cha afya kulikuwa na Zahanati tu.
"Sasa tunashukuru serikali kuu kueta shilingi 250 za ujenzi wa jengo hilo hivyo tunashukuru kwa uwepo wa kituo hiki"amesema Magangila.
"Sasa tunashukuru serikali kuu kueta shilingi 250 za ujenzi wa jengo hilo hivyo tunashukuru kwa uwepo wa kituo hiki"amesema Magangila.



0 Comments