WAKAZI wa kata ya Ikinda na Bugarama Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameondolewa kero ya kushindwa kupitia kwenye eneo la barabara ya Ikinda kwenda Bugarama ikihitaji ujenzi wa daraja kuvuka wakati wa mvua.
"Mradi huu nimeufungua kwani changamoto zilizokuwa zikiwakabili zimeondoka hakuna budi kuendelea kuwa watulivu na kuendelea kuitunza amani ya nchi kwani amani ikikosekana na daraja likawepo ni kazi bure"amesema Mwang'onda.
Meneja wa Wakala wa Barabara mjini na Vijijini (Tarura) wilaya ya Kahama Mhandisi Joseph Mkwizu akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge amesema mradi wa ujenzi daraja hilo ulianza rasmi mwaka 2025 mwezi Septemba na kukamilika mwezi Julai mwaka 2026.
Mhandis Mkwizu amesema daraja hilo lina urefu mita kumi na moja,upana mita nane ambapo ujenzi wa wake umekwenda sanjari na kuweka makaravati matatu ,kunyanyua tuta na kuweka molamu urefu wa kilomita moja na kuchonga barabara kilomita moja.
"Gharama ya mradi wote ni shilingi Milioni 410 na kukosekana kwa daraja kulisababisha wananchi kushindwa kuvuka na kusafirisha mazao yao na shughuli zingine za kibiashara na kijamii"amesema Mhandis Mkwizu.


0 Comments