WANANCHI WA KIJIJI CHA NSUNGA USHETU WAANZA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI KISIMA KIREFU


 
Na  Kareny  Masasy, Ushetu

WANANCHI wa  kijiji Nsunga  kata ya Uyogo Halmashauri ya Ushetu  Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wameanza kunufaika na mradi wa maji  wa chanzo cha kisima kirefu ambacho kinatoa lita 2,200 kwa saa.

 Hayo yamesemwa leo na  Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa  Wazo Mwang’onda   baada ya kuzindua mradi huo  ambao umewaondolea adha wanachi kwa kutumia maji machafu  yasiyo salama huku akisisitiza viongozi wa kata  wahimize wananchi  upandwaji wa miti kandokando ya kisima hicho ili kiwe endelevu.

Mwang’onda amesema chanzo cha   kupatikana maji hayo ni kisima kirefu ambapo serikali imejitahidi kuwanufaisha wananchi wake kwa kutoa  fedha nyingi kuhakikisha maji yanapatikana kwenye kijiji hicho.

“Rais Samia Suluhu  ni  Rais wetu nani mama ambaye ametaka kuhakikisha anamtua mama ndoo  kichwani ndiyo adhima yake na ndiyo maana amesogeza huduma ya maji karibu na wananchi  kwenye maeneo yao.”amesema  Mwang’onda.

Mbunge wa jimbo la  Ushetu  Emanuel Cherehani amesema  jimbo hilo lilipata fedha shilingi bilioni 44 kwaajili ya kutekeleza mradi  wa maji kutoka ziwa victoria ambao wanaendelea nao mpaka sasa.

“Juhudi zinafanyika kuhakikisha   maji yanapatikana kwenye maeneo yote ya ushetu  tunampongeza Rais kuendelea kutushika mkono kwa kutoa fedha na kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Maji,Elimu na Afya”amesema Cherehani.

Hata hivyo Meneja  wa Wakala wa maji na Mazingira vijijini (Ruwasa) Wilaya ya  Kahama  Mhandisi Magoli Maduhu amesema  Mradi huo umegharimu  zaidi ya shilingi Milioni 82.6 nakuwanufaisha  wananchi 1,092.

Mhandisi Maduhu amesema  kisima kirefu chenye  urefu wa mita  40 na uwezo wa kutoa  lita hizo kwa saa na ujenzi wa mnara  kioski  cha kuchotea maji na kusimika tanki,

Post a Comment

0 Comments