KIONGOZI wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Wazo Mwang'onda ameweka jiwe la msingi jengo la vyumba vitatu vya madarasa kwenye shule ya sekondari Kagongwa iliyopo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.
Shule hiyo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi kuchangia shilingi Milioni saba huku ukamilishaji wake ukitolewa na halmashauri ya Manispaa fedha za mapato ya ndani shilingi Milioni 63.
Mwang'onda amesema hayo leo baada ya mwenge wa Uhuru kupokelewa katika viwanja vya shule ya sekondari Kagongwa ukitokea Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga huku mkuu wa Wilaya ya Kahama Frank Nkinda akikabidhiwa.
Mwang'onda amesema amefurahishwa na ujenzi huo pamoja na ushirikishwaji wa wananchi lakini amekubali kuweka jiwe la msingi na imefikia hatua ya ukamilishaji nakuwataka wazazi wawasimamie watoto wao maendeleo ya shule ili wafaulu masomo yao.
Mwang'onda amesema shule hiyo ameipatiwa cheti kwaajili ya klabu ya wapinga rushwa kwa wanafunzi 60 ambao wanachama wa klabu hiyo iliyoanxishwa mwaka 2023 na wanaendeleza mapambano ya kupinga vitendo vya rushwa. na hiyo ndiyo inatakiwa ili Tanzania iendelee kuwa salama.
"Nimezindua upandaji wa miti kwenye shule hiyo hali ambayo inatakiwa mazingira kutunzwa na kusimamiwa vizuri na kila mwanafunzi anatakiea awe na mti wake wa kutunza ikikua hata mazingira ya kujisomea yatakuwa mazuri"amesema Mwang'onda.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda wakati wa kupokea mwenge huo kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro amesema mwenge huo utakimbizwa halmashauri tatu za ushetu,Msalala na Kahama kwa kupita kwenye miradi 21 yenye thamani zaidi ya shilingi bilion 5.4 na kukimbia umbali wa kilomita 361.4




0 Comments