MKURUGENZI WA MANISPAA YA KAHAMA APONGEZWA KWA KUVUKA LENGO USAJILI WA VIKUNDI KWENYE MFUMO WA NeST


Na Kareny  Masasy, Kahama
  KIONGOZI wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa  Wazo Mwang’onda  amempongeza   Mkurugenzi  wa Manispaa ya Kahama   Mkoani Shinyanga Masudi Kabetu  kwa  kuvuka lengo la  kuwa na vikundi 326  sawa na asilimia 217.

Mwang’onda amesema hayo leo  baada ya kusikiliza taarifa  ya usajili na ushiriki wa makundi maalum kwenye Mfumo wa Manunuzi wa Umma  kwa njia  ya kielektroniki ( NeST) kwenye eneo la mkesha wa Mwenge  alipotembelea banda la Mamlaka ya udhibiti wa Manunuzi wa Umma (PPRA)  katika viwanja vya stend ndogo ya Malori  kata ya Majengo.

 Mwang’onda ametoa pongezi hizo  baada ya kuona  lengo lililopangwa kitaifa kwenye halmashauri hiyo ni  kusajili vikundi 150  lakini imekuwa zaidi ya mara mbili nakueleza huo ndio uongozi uliotukuka  kwa kusimamamia jamii iweze kunufaika na fedha zinazotolewa na serikali yao.




Ofisa  Maendeleo ya jamii  Manispaa ya  Kahama Mbwana Karata  alimueleza kiongozi huyo kuwa  halmashauri ilikuwa imesajili makundi maalum kwenye mfumo wa  ununuzi wa umma wa kielektroniki.

“Lakini  hadi sasa vikundi vilivyosajiliwa  ni 326  sawa na asilimia 217 kati ya makundi hayo vikundi 173 ni vya vijana,vikundi 150 vya  wanawake , vikundi viwili ni vya watu wenye ulemavu na kikundi kimoja cha wazee”amesem Karata .

Karata amesema halmashauri imetenga zabuni za  zaidi ya shilingi  bilioni 1.9 fedha ambayo ni bajeti ya asilimia  30 ya manunuzi ya serikali.

“Hadi sasa vikundi vinne vimetunukiwa zabuni zenye thamani  ya zaidi ya  shilingi  Milioni 242.45  kati ya hivyo vikundi vya  vijana viwili vilipata zaidi ya  shlingi  Millioni 74.4 na  vikundi viwili vya  wanawake shilingi Milioni 168”amesema Mbwana.

 





Post a Comment

0 Comments