Na Mwandishi Wetu,
JENGO la Waraibu wa madawa ya kulevya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga limekamilika kwa asilimia 100 ambapo limetumia shilingi Milioni 438 fedha kutoka serikalini kwa kushirikiana na wadau.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Wazo Mwang’onda amepongeza kuwepo kwa jengo hilo leo alipokuwa akizindua huku akieleza litasaidia kutoa huduma kwa waraibu hasa vijana ambao wamekuwa wakiharibiwa na madawa ya kulevya.
“Ninawaomba vijana achene kujihusisha na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya yanawapotezea dira ya maisha na nguvu kazi kwa taifa anawashauri vijana wafanye kazi halali zenye kuwaingizia kipato”amesema Mwang’onda
“Vijana wenzangu tukiwa na tabia njema na kujishughulisha hata Rais wetu Samia Suluhu Hassan ambaye ni mama ataendelea kufurahi na kutuwekea mikakati ya namna ya kutuinua kiuchumi zaidi tuchukulie mfano wa mama zetu nyumbani tukifanya vitu kinyume huwa wanasikitika ndiyo ilivyo kwa serikali hivyo tuendelee kumfurahisha mama”amesema Mwang’onda.
Mganga mkuu wa Manispaa ya Kahama Baraka Msumi akitoa taarifa kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa amesema jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2025 na limekamilika nakuratajia kuhudumia waraibu wa madawa ya kulevya




0 Comments