Na Mwandishi wetu, Bukombe
Amani ni urithi mkubwa wa Tanzania na msingi wa maendeleo yanayoendelea kushuhudiwa nchini.
Kauli
ahiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe na aliyekuwa Naibu
Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko, wakati wa ibada na mazishi ya aliyekuwa
Diwani wa Kata ya Ilolangulu, Kabula Ndabacha, yaliyofanyika wilayani
Mbogwe.
Kutokana
na haja hiyo amewataka Watanzania kuendelea kuenzi na kuudumisha
utamaduni huo wa upendo, umoja na mshikamano akisisitiza kuwa misingi
hiyo ni nguzo muhimu ya maendeleo endelevu ya Taifa.
Dkt.
Biteko amesema nyakati za mafanikio na changamoto zinahitaji wananchi
kuendelea kuthaminiana, kusaidiana na kuishi kwa upendo bila kujali
tofauti zao. Aidha, ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa,
marafiki na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema kifo cha
Ndabacha ni pigo kubwa kwa familia, wananchi wa Kata ya Ilolangulu na
chama hicho kutokana na mchango wake katika kuwatumikia wananchi.
Amewataka
wananchi wote kuendeleza mema yote yaliyoachwa na marehemu kwa
kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, kuimarisha mshikamano
na kulinda amani ambayo imekuwa tunu na fahari ya Tanzania.

0 Comments