Na Kareny Masasy, Kahama
MKURUGENZI wa shule za Anderlek Ridges na Rocken Hill Sir Alexander Kazimili amewafunda vijana wote nchini kutumia Akil unde kama fursa ya kujiajiri nakuongeza kipato katika maisha yao hakuna maisha mazuri yatakayokuja bila kuwa na ubunifu.
Kazimili amesema hayo leo kwenye mahafali ya shule ya sekondari Anderlek Ridges na shule ya msingi Rocken Hill zilizopo Mansipaa ya Kahama mkoani Shinyanga ambapo amewaeleza vijana lazima waijue dunia ya utandawazi yenye ubunifu na ushindani .
Kazimili amesema wanataka waone vijana wanashindana kimataifa kwani dunia ya leo haimpi nafasi mtu ambaye ni dhaifu,hajitambui,mzembe ,hana ndoto yoyote na hafanyi bidii katika kazi.
“Mimi nilianza ujasiriamali na kufundisha nikiwa bado shuleni na ndiyo ilikuwa ndoto yangu na leo imetimia unatakiwa maono yako uyaanze chini na kwenda juu lakini wengine huanzia juu kwenda chini na mambo ya akili unde yatumike kama fursa imekuwa tofauti vijana wanatumia kwenda kinyume na maadili”amesema Kazimili .
Kazimili amesema Maadili kwenye jamii yamemomonyoka kwani vijana siku hizi wamekuwa wakiwatishia hata wazazi wao kutokana na dunia inavyowapeleka hivyo wengi wao wamekuwa waathirika wakubwa sana kufikia hatua kuwaomba urithi wa mali.
Mgeni rasmi aliyesoma shule hiyo na sasa ni daktari wa magonjwa ya Moyo Nchini Urusi na Mwalimu wa Chuo Kikuu Joseph Charles amesema ushuhuda uliopo mkurugenzi wa taasisi hii ametumia maono na ujasiri mpaka amepiga hatua ya mafanikio na sasa anajivunia.
Dkt Charles ameelezea historia ya uanzishwaji wa shule hiyo amesema ilianza mwaka 1999 na kulikuwa na jengo moja la madarasa mawili na ofisi moja hivyo ni suala la kujivunia taasisi hiyo kwa kupiga hatua kubwa kwa maendeleo yaliyofanyika na kukua kwake na kutambulika.
“Tunaona hii leo ni mtu mmoja alikuwa na maono na ujasiri mkubwa sana hivyo haikuwa rahisi mara nyingi binadamu huanzia chini na mwanzo wake unakuwa mgumu kwa kukutana na vikwazo”amesema dkt Charles.
Dkt Charles amesema ukiamini kitu na kukiweka kwenye maono na bidii ya kazi ni lazima ndoto itimie hivyo ninampongeza mkurugenzi kwa kutokata tamaa na kutimiza ndoto yake ambayo leo tunaishuhudia.
Dkt Charles amesema wanafunzi kwa elimu waliyopita watabadilisha maisha kwa kupata maarifa na sio ufaulu wa mitihani na safari yangu ilianza shule ya msingi Rocken Hill na leo hii nimefika Urusi kama daktari wa magonjwa ya moyo.
Dkt Charles amewahasa wanafunzi waendelee kuwasikiliza walimu na kuwa na bidii ili kuweza kutimiza ndoto zao na eneo la shule sio kufaulu mitihani bali linawajengea uwezo wa kwenda kufanya kazi na kulitumikia taifa.
Mkurugenzi wa shule za msingi za Rockeni Hil Zephania Maduhu amesema maandalizi ya wanafunzi hawa ni safari ndefu imetumika na kuwa thabiti katika kuwaandaa hadi hatua waliofikia ya kutarajia kufanya mitihani ya taifa na wamefundishwa katika misingi bora ya maadili .
Mkurugenzi
wa shule ya sekondari ya Anderlek Ridges Godwin Ng’osha amesema kwa sekondari ni mahafari ya 21 kwa wanafunzi kidato cha nne na
amewahasa wanafunzi kutumia teknolojia vizuri nasio kuharibu maisha yao
na wazazi wasitetee watoto
wanapohalibu bali waonywe nakufundishwa
0 Comments