WAZIRI NDEJEMBI AUNGA MKONO NA KUTOA USHAURI UTEKELEZAJI BARABARA KAHAMA KWENDA KAKOLA

Na  Kareny Masasy,Kahama
 
 WAZIRI wa Nishati nchini Deogratias  Ndejembi amesema  Mkandarasi wa ujenzi wa barabara  ya kahama  kwenda Kakola  yenye urefu wa kilomita 73 aongeze kasi ya ukamilishaji huku akiunga mkono  uwekwaji wa  taa za barabarani pindi itakapokamilika.

Waziri  Ndejembi  ambaye ni mlezi wa mkoa wa Shinyanga  amesema  hayo leo  alipofanya ziara ya kutembelea mradi wa kimkakati  wa barabara inayojengwa kiwango cha lami  inayosimamiwa na serikali kwa  ufadhili wa kampuni ya Barrick Gold Mine  kwa gharama ya  bilioni 100.6 na kujengwa na Kampuni ya China Civil  Engeneering Contruct Ltd (CCEC).

Waziri Ndejembi amesema   amekuja  kukagua  na kuona ilani ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kwenye miradi ya kimkakati ambapo mojawapo ni barabara  hii ambayo alisisitiza mkandarasi aongeze  kasi ya utekelezaji ili kufikia mwezi Septemba mwaka 2026  kwa mujibu wa mkataba ulivyo  awe amekamilisha.

“Nimesikia kilio cha wananchi  kuhusu mahitaji ya taa za barabarani    na kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo ambapo mazungumzo yanafanyika ili kuondoa changamoto waliyonayo”alisema  Ndejembi.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Mboni Mhita amesema  barabara hiyo kipindi kirefu  miundombinu yake ilikuwa ni  vumbi na  kwenye uongozi wa  awamu ya sita Rais Samia Suluhu alitoa fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo   na maelekezo  juu ya usimamizi wa miradi ya kimkakati. Mbunge wa jimbo la Kahama mjini  Benjamini Ngayiwa  amesema ukamilikaji wa barabara hiyo itakuza uchumi kwenye majimbo mawili kwa kurahisisha usafiri pia aliomba mkandarasi huyu ndiye anayetekeleza miradi ya TACTICS  kwa ujenzi wa barabara na soko hivyo aongeze kasi ya  ujenzi. Mbunge wa jimbo la  Msalala Mabula Magangila ameomba   maeneo ya wachimbaji wadogo yapatiwe nishati  ya umeme kwani wanatumia dizeli kwenye shughuli za uchimbaji wanapata hasara kutokana na bei ya mafuta kubadilika badilika  mara kwa mara na  gharama  inakuwa  kubwa.

“Jimbo  hili lina kata  18 ambapo kata  12  zinazungukwa na shuguli za uchimbaji madini na kata nne ziko kwenye utafiti hivyo uwepo wa barabara ya kiwango cha lami ni hatua ya  kuwavutia wawekezaji  na kukuza uchumi kwa wachimbaji wadogo”amesema Magangila.

Magangila amesema  Halmashauri ya  Msalala  kipato chake kwa mwaka mmoja sekta ya madini pekee huchangia shilingi biloni 120 kwenda kwenye mfuko wa serikali  ni vyema sasa kuona umuhimu wa taasisi kama vituo vya afya,Zahanati, Shule na nyumba za ibada kuna nishati ya umeme. Meneja wa Wakala ya Barabara  (Tanroads) mkoa wa Shinyanga Mhandis Ntuli  Mwaikokisye  amesema ujenzi wa barabara hiyo ulianza mwaka 2024 na mkataba wake ni miezi 27  na tayari amekamilisha  kilomita 33 kati ya kilomita 73 zinazohitajika kiwango cha lami. 

Post a Comment

0 Comments