Na Kareny Masasy, Shinyanga
WAKAZI
zaidi ya 20,000 kutoka kata za Imesela na Bukene Halmashauri ya wilaya
ya Shinyanga wameanza kunufaika na mradi wa maji safi baada ya shirika
lisilo la kiserikali la Water for Good kwa kushirikiana na Wakala wa
Maji safi na Mazingira vijijini (Ruwasa) kutekeleza mradi wa
usambazaji maji.
Hayo
yamesemwa na Mhandisi wa maji wa Shirika hilo Raphael Lwassa
walipokuwa wakikagua tank la maji lenye ujanzo wa mita 100 lililojengwa
kwenye kijiji cha Zumve kata ya Nyamalogo halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga kwa lengo la kusukuma maji.
Mhandisi
Lwassa amesema mradi umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.1 ikiwa
ulianza utekelezaji mwaka 2024 nakutarajiwa kukamilila mwezi Disemba
mwaka 2026.
Mhandis
Lwassa amesema bomba la mtandao wa kilomita 44 limezamishwa kwaajili
ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya jua kupeleka kwenye vijiji
vitatu vya kata ya Bukene ambavyo ni Simbigu, Bukene na Masekelo .
Mhandisi
Lwassa amesema mradi huo kwa kata ya Bukene unajumuisha kituo cha
kusukuma maji kinachotumia nishati ya jua na tanki la kuhifadhi maji na
vituo 31 vya kuchotea maji .
"Mradi
unawafikia wakazi 11,668 kutoka kata ya Imesela na kutoka kata ya
Bukene inawafikia wakazi 8,106 ambao wanapata maji safi na salama
kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022"amesema Mhandisi
Lwassa.
Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Water for Good Dave Levan amesema wamefurahi kutekeleza
mradi kwa ushirikiano na kusisitiza kuendelea kutekeleza miradi mingine
zaidi kwenye halmashauri kwaajili ya kusaidia wananchi na utunzaji wa
mazingira.
Meneja wa
Ruwasa Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliette Payovera amesema shirika
hilo walianza kufanya nalo kazi mwaka 2021 kwa kutekeleza miradi ya
maji kwenye maeneo mbalimbali ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Mhandisi
Payovera amesema Mradi huu ambao ni usambazaji wa maji kwenye vijiji
vinne ni awamu ya pili na wadau wametoa fedha kwa asilimia 62 na
serikali kwa asilimia 28 na eneo limetolewa na wananchi wa kijiji cha
Zumve.
Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Julius Mtatiro amesema mradi huo unatakiwa ulindwe na utunzwe
kwani umesaidia wanawake na watoto kuondokana na adha ya kutembea umbali
mrefu kutafuta maji ndoa zilivunjika na wanafunzi kukatiza masomo yao.



0 Comments