TRA KAHAMA YAANZA SHAMRA SHAMRA KUSHEREKEA MIAKA 30


                        Na Kareny  Masasy, Kahama

MAMLAKA ya Mapato  Tanzania (TRA) Mkoa wa wa kikodi Kahama   umejumuika na   Kahama club  Jogging   kwa kusherekea miaka 30  nakufanya mazoezi  huku ikipanda miti kwenye shule ya sekondari Kishimba iliyopo Manispaa ya Kahama.

Watumishi wa Mamlaka hiyo  leo  wakiongozwa na Meneja wa TRA kahama  Wisaka  Kamwamu  walifanya mazoezi hayo majira ya asubuhi  kwa kuzunguka kwenye  barabara za mitaa  nakuhamasisha suala la ulipaji kodi na utunzaji wa mazingira.

Kamwamu amesema katika kusherekea  miaka 30 ya kuanzishwa kwa TRA  wameona ni vyema  wakajumuika na   kundi la club jogging ambao nao ni walipa kodi ili kuendeleza zoezi na utoaji elimu kwenye jamii na watumishi kuendelea kuwa na afya nje na kutumikia tafa.

“Mimi leo nimefurahi sana Kahama Club jogging tutakuwa pamoja katika ushirikianao nasi   mkitutaka katika kushiriki kwenye mazoezi tuko tayari hata taasisi zingine kwani tuko hapa kuijenga nchi yetu  kwa kulipa kodi  kwa umoja upendo na mshikamano” amesema Kamwamu.

Pia Meneja aliongozana  na Watumishi  wa TRA kupanda miti kwenye shule ya sekondari  Kishimba  huku akieleza wameona wampande miti ili kutunza mazingira kwenye shule hiyo  kwani waliangalia  shule iliyopo karibu ingawa zipo shule nyingi na walichagua shule hiyo kuhakikisha miti waliyopanda inastawi vizuri nakutambua vijana wakikua watakuwa wlipakodi wazuri.

“Tunajivunia miaka 30 ya TRA na miaka  mitatu  mfululuzi  Kahama tumekuwa tukifanya vizuri  tunatembea kifua mbele  kwa kuona jamii inatambua ulipaji kodi” amesema  Kamwamu.

Mwenyekiti wa Club ya Jogging Kahama  Abdallah  Mmagane wameona kusaidia serikali  kuhamasisha mazoezi ili wananchi waweze kupunguza maradhi mbalimbali kama  vile shinikizo la damu,kisukari  na Mazoezi yanafanywa na mtu yeyote na mwenye umri wowote  pia mtu akijumuika atapunguza mawazo na kupata mtandao na watu wengine .

Makamu wa Shule ya sekondari  Kishimba  Mwalimu Adelina Masawe amesema  shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 1000 na walimu 52 hivyo wanahitaji sana miti ipandwe ili kuwepo na hewa safi na kivuli kwaajili ya wanafunzi wanapokuwa kwenye mazingira haya nakujisomea pia.





 

Post a Comment

0 Comments