Na Kareny Masasy, Shinyanga
MPANGO shirikishi na endelevu wa utoaji wa elimu ya afya ya jamii na kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto umeendelea kuondoa changamoto zilizokuwepo na zinazoibuka kwenye jamii katika Kjiji cha Sayu Kata ya Pandagichiza wilayani Shinyanga.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mtendaji wa kata ya
Pandagichiza ambaye ni mtendaji wa kijiji cha Sayu Rwambo Mayanzani alipokuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mpango shirikishi wenye mambo manne ulioanzishwa na mwananchi wa kijiji hicho
Shadrack Dasea baada ya kupata kibali kutoka
serikalini.
Mayanzani amesema wameungana na mwananchi huyo kwani kitu alichokianza na mawazo yake ni mazuri ambapo wamekuwa wakitoa elimu ya afya kwa jamii na kutokomeza vitendo vya ukatili kwa kupita kwenye nyumba za ibada,shuleni na sokoni.
“Elimu ya ukatili imeendelea kutolewa kwa watu wote baada ya kuona wahanga zaidi walikuwa wanawake na watoto lakini ukatili umeenda ukipungua wanaume nao kuelimika ndani ya familia zao”amesema Mayanzani.
Mwanzilishi wa mpango huo ndani ya kijiji Shadrack Dasea ameamua kuanzisha mpango huo baada ya kuguswa kwa kuongezeka kwa matukio ya ukatili ndani ya jamii huku akiamini kuwa akitoa elimu hiyo itasaidia kuboresha ustawi wa wananchi.
Baadhi ya
wananchi wa kijiji hicho Verena Mihambo na Laurent
Kongoshi waliohudhuria uzinduzi wa mpango huo wameeleza kuja kwa wakati
sababu viashiria vyote vya masuala ya ukatili kwa
wanawake na watoto wanaendelea kuvitokomeza kwa ushirikiano.
Ofisa
Maendeleo ya Jamii mkoa wa
Shinyanga Bestina Gunje alieleza Mpango
Mkakati wa Mkoa na Mpango Mkakati wa Taifa wa kutokomeza ukatili kwa Wanawake na Watoto ( Mtakuwwa) umefanikiwa kupunguza tatizo la ndoa za utotoni kutoka asilimia 35
hadi asilimia 21.
“Mpango Mkakati wa Taifa ulioanza mwaka 2023 nakuisha mwaka 2024 na hapa Shinyanga mpango wetu uliopo umeendana na mazingira ya mkoa yalivyo ambao ulianza mwaka 2021 nakuisha mwaka 2025 tulikuwa na changamoto ya ndoa za utotoni asilimia 35 na sasa tumeshuka nakufikia asilimia 21 hayo ni mafanikio makubwa kwetu”alisema .
Mwenyekiti wa Umoja wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Shinyanga yanayopambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (SHY-EVAWC Working Group) Jonathan Manyama aliyeshiriki kwenye uzinduzi huo alisema vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia vinapaswa kupingwa na watu wote na kuacha tabia ya kuendeleza vitendo vya ukatili.
0 Comments