Ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa kikodi Kahama umeeleza kutatua changamoto hizo kwani nao ni sehemu ya jamii wanaotakiwa kuishi maisha mazuri kama watu wengine.
Walezi wa kituo hicho Agata Charles na evarist Masanja wameeleza changamoto hiyo leo mbele ya Meneja wa TRA Mkoa wa kikodi Kahama Wisaka Kamwamu alipokuwa ameambatana na baadhi ya watumishi walipokuwa wakikabidhi msaada wa vyakula,vinywaji, sabuni ikiwemo shilingi 500,000 tasilimu.
Charles amesema kuna watoto 50 ambapo wasichana ni 30 na wavulana ni 20 ikiwa wote wanasoma madarasa tofauti kuanzia awali hadi sekondari waliletwa kwenye kituo hicho wakiwa yatima na wengine waliokuwa wakiishi kwenye mazingira magumu.
Masanja amesema changamoto iliyopo watoto hao hawana bima za afya hali wakiugua inakuwa changamoto kupata fedha za matibabu pia aliomba wapatiwe solar ili siku ukikatika watoto waweze kujisomea na kuongezewa jiko la gesi kwani ikiisha kuweka inakuwa hakuna fedha nakufika hatua ya watoto kutaka kulala njaa.
“Tunashukuru kwa msaada mkubwa mlioutoa tunaomba mkienda huko mtuangalie suala la mahitaji mengine ikiwemo vyombo vya kupikia kama sufuria zimekuwa za siku nyingi ni chakavu”amesema Charles.
Meneja wa
TRA Wisaka Kamwamu
amesema wameamua kutoa msaada wa vitu hivyo na fedha
kwa kusherekea miaka 30 ya tangu
kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo nchini ambapo
hawataishia hapo wamesikia
changamoto zilizopo nakwenda kuanzisha
harambee ili kuweza kuzitatua.
“Kama suala
la bima ya afya na gesi ya kupikia hilo suala tumelichukua nakulifanyia
kazi najua kwa mapenzi ya mungu
hamtaweza kulala njaa na hakuna
budi sisi kama watumishi kuhudhuria
kwenye kituo hiki mara kwa mara”amesema Kamwamu.
Kaimu Meneja Msaidizi Mkoa upande wa ukaguzi TRA Kahama Ester Martin amesema watoto hawa ni upande wa jamii wakikua ni walipa kodi wazuri hivyo wamekuja kuwaona na wapo waelewa na kipindi hiki wako karibu na walipa kodi nakushirikiana nao ili wafahamu takwa la kisheria na ulipaji kihiari.

0 Comments