
Na Kareny Masasy,Shinyanga
KANISA la Angilikana Tanzania Dayosisi ya Shinyanga imezindua rasmi mradi wa malezi na makuzi ya mtoto utakaotekelezwa wenye lengo la kuboresha maendeleo ya awali ya ukuaji wa mtoto kupitia malezi bora,ushiriki wa jamii na kuimarisha ustawi wa uchumi wa kaya.
Askofu wa kanisa la anglikana Tanzania dayosisi ya Shinyanga Johnson Chinyong’ole amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi huo utakaotekelezwa katika halimashuri ya wilaya ya Kishapu katika vijiji vya Mayanji, Bulimba, Mwaweja na Negezi
Askofu Chinyong’ole amesema utekelezaji wa mradi huo ni agizo la Mungu kwani Yesu alisema amekuja duniani ili watu wawe na uzima tele hivyo uzima ni pamoja na ustawi wa afya njema.
Askofu Chinyong’ole amesema mradi huo unaenda kutekelezwa kwa kushirikiana na jamii pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya afya ili kuendelea kuongeza uelewa kuhusu malezi mazuri ya watoto pamoja na haki zao ili kuboresha mazingira ya ukuaji.
“Kupitia mradi huu tunatarajia kuona ongezeko la uelewa wa wazazi na walezi kuhusu malezi bora kwa watoto ikiwa ni pamoja na kuboreshwa kwa afya na lishe ya watoto kuimarika katika mkoa wa Shinyanga “amesema Hamduni.
Hamduni
amesema mradi huo unakwenda sambamba na jitihada za serikali ya
awamu ya sita katika kuboresha huduma za awali za maendeleo ya mtoto kwa
kuhakikisha watoto wanapata huduma za afya na lishe bora kwa kuzingatia
ustawi wa afya ya mwili na akili pia.
Mganga mkuu
mkoa wa Shinyanga dkt Honaratha
Rutatinisibwa amesema kupitia mradi huo jamii inakwenda kujengewa uelewa
mkubwa kuhusiana na malezi ya mtoto na kwamba utakwenda kupunguza tatizo
la udumavu pamoja na kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto.
Uzinduzi wa mradi huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo, afya na makuzi ya mtoto na unatajwa kuwa chachu ya kuongeza uelewa wa malezi bora na yenye usatwi kwa mtoto katika jamii.
0 Comments