WASANII wa muziki kumi kutoka nchini wakiongozwa na msanii wa kike Nandy wanatarajia kuja mkoani Shinyanga kwaajili ya kutumbuiza na kuwapatia burudani wananchi wa mkoa huo mnamo tarehe 20 mwezi Juni,2026.
Wasanii hao wakiongozwa na Msanii wa kike Nandy ambaye amebeba tamasha hilo linalojulikana kama NANDY FESTIVAL 2026 kwa kusherekea miaka 10 yakuwepo kwenye tasnia ya muziki.
Mwakilishi wa NANDY FESTIVAL 2026 Remmy Nguvu akiongea kwenye uzinduzi wa tamasha hilo lililo dhaminiwa na Jambo Group (JAMUKAYA) amesema wameamua kuanza na waendesha daladala za baiskeli kuwapatia pampu kama zawadi na kuwa sehemu ya kuhamasisha na kusafirisha wananchi kuwaleta kwenye burudani.
Nguvu ambaye mwakilishi wa Msanii Nandy akishirikiana na Jambo Media na Jambo Group maarufu (Jamukaya) wakati akigawa pampu za baiskeli bure kwa waendesha daladala za baiskeli.
“Tumeona waendesha daladala za baiskeli ni miongoni mwa
wadau muhimu wanaosaidia wananchi kufika maeneo mbalimbali kwa gharama nafuu na
kuona ni muhimu kuwapongeza kwa mchango wao kupitia
zawadi hizi za pampu za baiskeli”amesema
Nguvu.
Nguvu amesema shughuli hiyo ni sehemu ya maandalizi ya NANDY FESTIVAL 2026, tamasha litakalokwenda sambamba na kusherehekea miaka kumi ya safari ya muziki wa Nandy, huku likitarajiwa kuwakutanisha maelfu ya mashabiki wa muziki kutoka maeneo mbalimbali.
Tamasha hilo linatarajia kufanyika Uwanja wa Shycom Juni 20, 2026 huku akiwaomba wananchi kwenda kushuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali watakaopanda jukwaani kama Billinas na Rayvann.
Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Group Renatus Kiluvia amesema hatua ya kuwapatia pampu waendesha dala dala za baiskeli inaonyesha namna NANDY FESTIVAL 2026 inavyothamini mchango wa makundi mbalimbali ya kijamii yanayowahudumia wananchi kila siku.
Kulivia amesema waendesha baiskeli hao wamekuwa na nafasi kubwa katika kurahisisha usafiri wa abiria kutoka sehemu moja kwenda nyingine, jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wengi wa Manispaa ya Shinyanga.
0 Comments