WATUHUMIWA 78 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI SHINYANGA

 

Na  Kareny Masasy,Shinyanga

JESHI la polisi mkoani Shinyanga limewashikilia  watuhumiwa  78   kwa makosa mbalimbali ya kiuhalifu  kati yao wahamiaji  haramu wakiwa kumi na moja  wanaoishi nchini bila vibali.

Kamanda wa jeshi la  polisi mkoani hapa  Janeth Magomi alisema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ambapo ameeleza   kushikiliwa kwa watu hao kulitokana na oparesheni maalum iliyoendeshwa kwa kipindi cha kuanzia mwezi  April hadi Mei mwaka 2026.

Kamanda Magomi amesema  oparesheni hiyo ilikuwa na lengo  la kuzuia  na kudhibiti  vitendo vya  uhalifu,kukamata wahalifu  pamoja na vielelezo  vinavyohusiana  na makosa  ya uhalifu.

Kamanda Magomi amesema  oparesheni hiyo  limefanikiwa  kukamata jumla  ya watuhumiwa  78 kwa makosa pia  kukamata silaha moja  aina ya  Bastola TISAS.

Kamanda Magomi amesema  silaha hiyo  yenye  namba za usajili  T0620-22J00122 ikiwa  na risasi 11 ndani  ya Magazine ambapo  iliripotiwa  kuibiwa katika tukio la wizi  lililotokea Mei 10,2026 katika  mtaa wa Nyakato wilaya ya Kahama.

Magomi ameeleza  silaha hiyo ilikuwa ikimilikiwa  kihalali  na Richard  Mhabi  (38) mfanyabiashara  mkazi wa Nyakato kahama ikiwa watuhumiwa wawili  wamekamatwa  kuhusiana  na tukio  hilo  na  wanashikiliwa kwaajili ya kuendelea na taratibu za kisheria.




Post a Comment

0 Comments