SHIRIKA LA WATER FOR GOOD LAWANUFAISHA WANAFUNZI MIUNDOMBINU YA VYOO SHULENI


Na Kareny  Masasy, Shinyanga

ZAIDI ya wanafunzi  600 wa  shule za  msingi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wamenufaika na huduma ya miundombinu  ya mazingira baada ya shirika la Water for Good  kujenga vyoo 22 vyenye   matundu 93.

Hayo yamesemwa leo   Mkurugenzi kutoka shirika la Water for Good nchini  Tanzania Devocatus  Kamara katika hafla ya makabidhiano ya miundombinu ya matundu ya vyoo 15 na machoteo ya maji 12 katika shule ya msingi Masekelo iliyopo kata ya Bukene Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Kamara amesema  walianza utekelezaji wa miundombinu hiyo kwaajili ya kuboresha huduma ya elimu na  mazingira kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kuanzia  mwaka 2021 hadi sasa  nakufanikiwa kutekeleza adhima hiyo kwa wananchi.

 “Makabidhiano ya leo yanaonyesha uwajibikaji  wa pamoja  nani sehemu ya  kuboresha huduma bora kwa jamii ikiwa  ushirika huu ni kutoka shirika la  Water for good kwa kuboresha mazingira kwa  kuchochea elimu”amesema  Kamara.

 

Mhandisi kutoka shirika la Water for Good  aliyekuwa msimamizi wa  mradi huo  Raphael  Lwassa  amesema walianza mwezi  Novemba 2025  ujenzi wa Matundu ya vyoo 15, koki 12 za kuchotea maji  na Matundu ya Vyoo  Zahanati ya Simbigu  uliogharimu  zaidi ya shilingi Milioni 56.

“Wakala wa Maji   safi na Mazingira vijijini  (Ruwasa) imekuwa ikitekeleza mradi wa maji kwenye vijiji vitatu  vya Sumbigu Masekelo na Bukene  kwa kuweka ghati lakini sisi Water for Good tumeweka koki kwa gharama ya shilingi Milioni 4.8,Matundu ya vyoo  shule ya msingi Masekelo  kwa shilingi  Milioni 32.5  na Matundu ya vyoo matano kwenye  Zahanati ya  kijiji cha Simbigu kwa shilingi Milioni 18”amesema  Mhandisi Lwassa.

Mhandisi  Lwassa amesema  upande wa  miundombinu ya matundu ya vyoo wanafunzi 223 wa kike  watatumia matundu ya vyoo nane ikiwa chumba kimoja nicha kujisriri na wavulana 211   matundu saba  huku wakifuata muongozo wa serikali  wa utumiaji Wash  na kuwajali watu wenye ulemavu.

 

Katibu tawala  mkoa wa Shinyanga Hamduni Salum  ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye makabidhiano hayo alisema   mradi huo  ambao uko tayari utakwenda kuwahudumia wanafunzi  kwa matumizi ya kutoa huduma  safi na kuboresha mazingira mazuri ya kujifunzia.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya  wilaya ya Shinyanga ambaye ni Ofisa Elimu Msingi Andrew Mitumba amesema mradi huu kwenye shule ya masekelo utathibiti  utoro na utaongeza ufaulu kwani wanafunzi  waliokuwa wakihangaika zaidi na wakati mwingine kupoteza masomo na jamii ione na ijifunze ujenzi wa vyoo kama hivi.  








 

Post a Comment

0 Comments