TAKUKURU SHINYANGA YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 21.8


 

Na  Kareny  Masasy,Shinyanga

TAASISI  ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoani Shinyanga  imefanikiwa kurejesha   zaidi ya shilingi Milioni 21.8  kupitia utekelezaji wa miradi   mbalimbali  ya Maendeleo  kwa kipindi cha miezi mitatu.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy  amesema hayo leo  alipokuwa akiongea na waandishi wa habari  wakati akitoa taarifa ya utekelezaji na ufuatiliaji kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi March 2026.

Kessy  amesema   kati ya fedha hizo  zaidi ya shilingi milioni  5.5 zimeokolewa  kupitia ujenzi wa shule mpya ya awali na msingi Tinde B iliyopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Kessy amesema  ofisi ya takukuru ilibaini zaidi ya shilingi Milioni 5.3 zilipaswa kulipwa katika Mamlaka ya Mapato (TRA) ikiwa ni kodi ya zuio na shilingi 223,950 ilikuwa ni fedha ya ushuru wa huduma  iliyopaswa kulipwa  katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

“Zaidi ya shilingi  9,672,000 zimeokolewa  kupitia uelimishaji kwa njia  semina iliyotolewa  kwa viongozi wa vyama  vya msingi vya kilimo na Masoko (Amco’s) kwa wilaya ya Kishapu vilivyokuwa vikidaiwa kwenye makampuni ya ununuzi  wa zao la pamba”amesema Kessy.

Kessy amesema baada ya ufuatiliaji  walibaini changamoto zilizochelewesha  fedha hizo kulipwa  na mapendekezo yalitolewa  na kufanya ufuatiliaji  na hatimaye fedha zote zililipwa  katika Mamlaka husika.

 

Post a Comment

0 Comments