Na Kareny Masasy, Kahama
Profesa
Shemdoe aliomba mtaalamu mshauri ahakikishe anasimamia vyema kwa wote
waliosaini mradi huo ili kuweza kuisha kwa wakati nakufikia kiwango
kinachostahili
WAZIRI
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi) profesa Ridhiki Shemdoe amesema hatavumilia kuona mradi wa
barabara Manispaa ya Kahama kuchezewa nakushindwa kukamilika kwa wakati
kama ilivyokuwa kwa mkandarasi wa awali kushindwa kutekeleza kwa
wakati.
Profesa Shemdoe
aliyasema hayo juzi kwenye hafla ya utiaji sain upya mkataba wa
umaliziaji ujenzi barabara na mitaro kupitia mradi wa uboreshaji
miundombinu ya miji Tanzania (Tactic) kwa Manispaa ya Kahama mkoani
Shinyanga utakao gharimu shilingi zaidi ya shilingi bilioni 25.
Profesa
Shemdoe alisema mkandarasi aliyepatikana ni kutoka kampuni ya China
Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) inayotekeleza ujenzi
wa barabara ya Kahama kwenda Kakola ni wazoefu hivyo wanaombwa
watekeleze kwa mujibu wa mkataba miezi nane kuanzia mwezi Juni mwaka
2026 hadi kukamilika Januari 2027.
Profesa
Shemdoe aliomba mtaalamu mshauri ahakikishe anasimamia vyema kwa wote
waliosaini mradi huo ili kuweza kuisha kwa wakati nakufikia kiwango
kinachostahili"Stavumilia
kwa yale yaliyotokea na sihitaji kuongeza muda kwenye mkataba na
tarura naomba wasimamie kwa ukaribu kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu
wa mkoa kwani kazi iliyopo ni ujenzi wa barabara za mjini kati (CBD)
urefu kilomita 12.03 ,barabara ya kuingia Zongomela kilomita 3.06
,Mitaro ya kutiririsha maji ya mvua kilomita 4.9 amesema Profesa
Shemdoe.
Akiongea kwa
niaba ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara mjini na Vijijini (Tarura)
Mhandisi Humprey Kanyenye amesema kampuni ya mkandarasi M/S Sichuan
Road and Brigde (group) Corporation Ltd ilikubaliana kwa mkataba
kujenga miundombonu ya barabara kwa zaidi ya shilingi bilioni 20.8 kwa
muda wa miezi 15 kuanzia Novemba 2023 hadi Septemba 2025.
"lakini
hakutekeleza na kupewa muda wa nyongeza ya kwanza naya pili licha ya
hivyo alipewa adhabu ya kushindwa kutimiza kazi na mkataba
ulisitishwa rasmi mwezi Januari mwaka 2026 kwa kuzingatia taratibu zote
za muongozo wa kimkataba"amesema Kanyenye.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amesema mkandarasi aliyekuwa
akitekeleza awali baada ya kusaini mkataba aliongezwa mara mbili
nakushindwa kukamilisha kwa wakati pia baadhi ya wanasiasa wakaona
kutumia changamoto hiyo kuanza kuichafua serikali kwa wananchi.
Mbunge
wa jimbo la Kahama mjini Benjamin Ngayiwa amesema ni miezi sita sasa
tangu uchaguzi mkuu ufanyike kipindi cha kampeni waliongelea suala la
barabara hadi kufika bungeni na leo hii utekelezaji unaanza hakuna budi
kuipongeza serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kuwajali wananchi
wake.
Mwakilishi
mkurugenzi mtendaji nchini Tanzania kutoka kampuni ya CCECC Wu Zegang amesema waondoe wasiwasi kwani wanao uhakika wa kukamilisha kwa wakati.



0 Comments