WAJUMBE SHIRECU WAPITISHA RASIMU YA BAJETI ZAIDI YA BILIONI 2.8


Na Kareny Masasy,Shinyanga

 WAJUMBE wa Chama Kikuu Cha Ushirika Mkoani Shinyanga (Shirecu)  wamepitisha rasimu ya  bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 2.8  kwa mwaka wa fedha 2026/2027 huku ikijizatiti kuanza  kukopesheka  kwenye taasisi za kifedha.

Wajumbe hao wamepitisha   bajeti hiyo leo tarehe 28/02/2026   baada ya Meneja  wa Shirecu Alpha  Makasi  kuwasomea  taarifa na rasimu  ya  bajeti  kwenye mkutano Mkuu wa 31  uliowakutanisha  wajumbe  202 kati ya wajumbe 214  waliokuwa wakitakiwa kuhudhuria kwenye mkutano huo.

Makasi  akisoma taarifa hiyo amesema wajumbe wakiridhia kupitishwa kwa bajeti zaidi ya shilingi bilioni 2.8  na kukopa kwenye taasisi za kifedha wataweza kutimiza adhima ya mipango ya kuendeleza biashara ya ununuzi wa mazao Mchanganyiko,uanzishwaji na kufufua kiwanda kipya cha kukamua mafuta ya alizeti na kuendeleza duka la pembejeo.

“Taasisi za kifedha zilikataa kabisa kutukopesha kutokana na kuwepo kwa vikwazo vya deni kutoka benki ya Uwekezaji ya (TIB) lakini sasa tumeanza kuonyesha uaminifu wa kulipa na kupata ruhusa ya kuendelea kukopesheka kwenye taasisi za kifedha zozote nchini”amesema Makasi.

Mwenyekiti wa bodi ya Shirecu Naomi Chaba amesema  kuna vyama vya ushirika (Amco’s) 107 na wanachama 7413 ambapo mpango ulioanza mwaka 2025 hadi  Februari  2026  wamefanikiwa kununua mazao Mchanganyiko kama choroko na dengu,kugawa kompyuta mpakato 50 nakutoa mafunzo,kukarabati shule ya sekondari Buluba  na kusomesha wanafunzi 28  wa kidato cha tano kwa awamu kwa gharama ya shilingi Milioni 45.

Mrajisi msaidizi  wa Ushirika mkoa wa Shinyanga Ibrahim  Kakozi amesema taasisi za kifedha   sasa zikae sawa kuwakopesha shirecu  huku akiwataka wajumbe waeleze yale ambayo wanataka yatekelezwe na yakikwama waihoji bodi  nakutoa ushauri zaidi nini kifanyike.

mwisho

Post a Comment

0 Comments