Na Kareny Masasy, Shinyanga
WADAU wa Kupinga vitendo vya ukatili manispaa ya Shinyanga wametoa msaada wa vyakula mbalimbali ikiwemo kilo 900 za mahidi na sukari kilo 145 katika shule ya msingi Iwelyangula huku wakiwashauri wazazi kuendelea kutoa mchango wa chakula shuleni.
Mkurugenzi wa shirika la Rafiki SDO Gerald Ng'ong'a kwa niaba ya wadau wa kupinga vitendo vya ukatili waliochangia vyakula hivyo alisema upatikanaji wa chakula kwenye shule hiyo uwe endelevu huku akiahidi kutoa kilo 100 za mahindi kila baada ya miezi mitatu.
Ngo'ng'a alisema wazazi wanatakiwa kuunga mkono juhudi hizi kwa kuchangia chakula na mikakati iwepo ya kila robo na utaratibu wa utumikaji wa vyakula shuleni hapo walimu washirikishe wanafunzi waone vimetumikaje.
"Leo linafanyika zoezi la uzinduzi rasmi wa chakula shule ya msingi Liwelyangula wazazi nasi tuchangie libaki jukumu la walimu kufundisha na watoto wetu wafaulu mitihani yao"amesema ng'ong'a.
Mwakilishi kutoka shirika la Invest in Children Society (ICS) linalojihusisha na masuala ya malezi na makuzi ya mtoto Lucy Maganga akieleza suala la mawasiliano alisema wazazi wengi wanakosa kuwa na mawasiliano mazuri na watoto hilo ndio gepu kubwa ambalo pia kushindwa kujua mahitaji muhimu ya shule
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Iwelyangula Lea Mzava alisema shule hiyo ina wanafunzi 452 na leo amefurahi maadhimisho ya siku ya wanawake na uzinduzi rasmi wa chakula shuleni hapa lengo lilikuwa kuhamasisha wazazi kuchangia chakula kwani robo ya wanafunzi ndiyo wamekuwa wakilipiwa chakula.
Mwenyekiti kamati ya shule Machibya James alisema kwenye vikao wamekuwa wakisisitiza wazazi kuchangia na sasa wanakuka na mpango mpya mzazi asiyechangia chakula atachukuliwa hatua.
Ofisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Shinyanga Nyanjura Kiyenze alisema wazazi upo umuhimu wa utoaji chakula shuleni wasipo kula shuleni ni chanzo cha kufanya vibaya darasani igeni mfano wa shule ya msingi Lubaga wazazi wanatoa chakula na wanafunzi wanafanya vizuri.
Mwakilishi kutoka idara ya Elimu Msingi Manispaa ya Shinyanga Francisca Msindu alisema Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya shule na kuhakikisha wanafunzi wa wanasoma katika mazingira mazuri nakuwataka wazazi wahakikishe chakula shuleni kinapatikana ili kuwaondolea sdha wanafunzi kushinda njaa.

0 Comments