.jpeg)

Na Kareny Masasy,
Kahama
KAMATI ya kudumu ya nishati na Madini imeeleza utekelezaji wa nishati ya umeme kwenye vitongoji vilivyokusudiwa una lizisha huku zamu ya kuanza kupata nishati ya umeme nyumba kwa nyumba utaangaliwa zaidi ili kufikia adhima ya mwaka 2034 maeneo yote yawe na nishati hiyo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Subira Mgulu ambaye ni mbunge wa jimbo la Bagamoyo amesema hayo juzi kabla ya uzindizi wa uwashaji wa nishati ya umeme kwenye Zahanati iliyopo kitongoji cha Mwaguhuma kata ya Mwakata Halmashauri ya Msalala na Mashine ya kusaga iliyopo Kagongwa.Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Mgulu amesema serikali imeendelea kusisitiza taasisi kama shule na Vituo vya kutolea huduma za afya viwe na nishati ya umeme kwani wananchi walikuwa wakiteseka sana na kutoa vilio vyao wanapotaka huduma ya kujifungua nyakati za usiku.
"Hili suala la ukosefu wa nishati ya umeme kwenye taasisi tumeanza kulifanyia kazi kwani vijiji vyote hapa kahama tumeelezwa vina nishati ya umeme kazi iliyobaki ni kuwasambazia wananchi kwenye maeneo yao" amesema Mgula.
Mgula amesema katika bajeti iliyopitishwa mwaka 2025/2026 ilikuwa imelenga katika kila jimbo vitongoji 15 vipate nishati ya umeme na leo hii kamati imekuja kukagua nakuona utekelezaji wake ulivyofanikiwa katika vitongoji vilivyoainishwa..
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala Wa Nishati ya Umeme Vijijini (Rea) Jones Olutu amesema eneo la wilaya ya Kahama ni miongoni mwa maeneo ya kimkakati na vijiji vyote 509 vya wilaya ya Kahama vinaumeme ambapo wameendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na matumizi salama na sahihi ya umeme.
"Kwa mkoa wa Shinyanga kuna vitongoji 2704 kati ya hivyo vitongoji 1180 ndiyo vinaumeme na vitongoji 1524 havina umeme lakini vitongoji 532 mkataba wake ulisainiwa mwezi Januari na wakandarasi wapo kwenye maeneo kwaajili ya kuanza utekelezaji hivi karibuni"amesema Olutu.
Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba amesema kufikia mwaka 2030 vitongoji vyote vitakuwa na nishati ya umeme na kuanza zoezi la kuunganishwa kwenye nyumba zao kwa gharama ya shilingi 27,000 kwa waishio maeneo ya vijijini ambapo matumaini wananchi wote wameelimika wananyumba za kisasa zinahitaji umeme.
Madiwani kutoka kata za Mwakata Ibrahimu Six na Diwani wa kata ya Kagongwa Ismail Masolwa wamesema changamoto iliyopo nguzo zinaletwa chache uhitaji ni mkubwa na maeneo mengine ya vitongoji ni umbali wa kilomita tisa hivyo wanaomba uunganishwaji wa haraka ufanyike kwenye vitongoji vyote.
.jpeg)



.jpeg)
0 Comments