WAKALA WA VIPIMO MKOANI SHINYANGA YATOA ELIMU MAONESHO YA SIDO KITAIFA

WAJASIRIAMALI  wadogo wanaotengeneza bidhaa   wanatakiwa  kupelekeka vipimo vyao  kwa Wakala wa vipimo (WMA)  ili kuweza kumlinda mlaji kupitia uhakiki na uthibiti wa vipimo wanavyovitumia katika biashara zao.

Kuhakiki kwa  vipimo ni kwa mujibu wa sheria  vya vipimo sura  namba 340  mapitio ya mwaka 2023.

Hayo yamesemwa leo  na Meneja wa vipimo mkoa wa Shinyanga Emmanuel Malanga  kwenye maonesho  ya tano ya kitaifa ya Maendeleo ya Viwanda  vidogovidogo  (Sido) yanayofanyika Manispaa ya Kahama.

“Wakala wa vipimo tunafanya  uhakiki katika maeneo mbalimbali ya  wafanyabiashara wakubwa na wadogo    hivyo katika maonesho haya wajasiriamali kweli wanatengeneza bidhaa zao wajitahidi  kufika kwa wakala wa vipimo  ili vipimo wanavyotumia vihakikiwe na viwe sawa kwamtumiaji”amesema   Malanga.

Malanga amesema  kumekuwa na mkakati wa kukagua mizani zote zinazotumika kwa wafanyabiashara   kwani baadhi yao sio waaminifu wamekuwa wakitumia njia mbalimbali za udanganyifu kwenye   mizani ili kumpunja mteja na mtu akigundulika kulingana na kosa atachukuliwa hatua.

“Mteja anayehitaji mtungi wa  gesi kwanza afahamu gesi inakilo yake na mtungi wenyewe una kilo yake na ahakikishe asichukue mtungi bila kupimwa uzito kwenye mizani  pia wanapima dira za maji na mita za umeme.”amesema Malanga.

Afisa vipimo  Mwandamizi  kutoka mkoani Shinyanga Happiness  Saronge amewashauri wajasiriamali wadogo wapeleke  mizani zao zihakikiwe kwanza nakuwekewa nembo ya utambuzi   ili kumlinda mlaji.

Saronge amesema  wapo wajasirimali wadogo wamekuwa wakitumia vipimo batili  wameendelea  kuwapa elimu namna ya kutumia vipimo vilivyo sahihi kwenye bidhaa zao wanazozitengeneza ili wafuate sheria na wazidi kuaminika na wateja






 


Post a Comment

0 Comments