AZANIA BENK IMEKUJA NA SKIMU YA SANVN

AZANIA benk  imekuja na mambo makubwa matatu   jambo la kwanza ni  ushauri na elimu ya uhifadhi, jambo la pili kufungua akaunt ya makundi mbalimbali hasa za makundi ya vijana na wanawake,jambo la  tatu mikopo mbalimbali  wakiwemo wajasiriamali.

Hayo yamesemwa leo na Meneja Mahusiano - bidhaa za rejareja  kutoka Azania Benk  Peter Maganga  kwenye maonesho ya tano ya kitaifa ya   Shirika la Maendeleo la viwanda vidogo ( sido) yanayofanyika Manispaa ya Kahama.

Peter anasema skimu ya SANVN VIWANDA  ni mpango  wa  uwezeshaji  wananchi  kiuchumi  ili   ujuzi,masoko na mitaji katika  miradi  midogo na ya kati (SMI) ambapo walengwa wa  mpango huu ni wajasiriamali wadogo na wakati kwenye  viwanda wanaojishughulisha  kwenye uzalishaji  wa bidhaa  ili  kuongeza mnyororo wa thamani.

Peter anasema Skimu  ya mpango huu  inataribiwa  na taasisi tano ambazo  ni  SIDO,AZANIA BANK,NSSF,VETA NA NEEC inawawezesha wananchi ujuzi na teknolijia,hifadhi ya jamii na mitaji ambayo ni mikopo ya kuendeshea,kununua mitambo kwa mashart nafuu.

MWISHO.


Post a Comment

0 Comments