NORAH AWA MISS SHINYANGA 2026 HOLYSIMILE YAPONGEZA KWA KUFANIKISHA

  
Na Mwandishi  Wetu, Kahama

TAASISI ya Holysimile kupitia jopo la majaji limemtangaza  mshindi wa Miss Shinyanga   Norah  Eustadius  ambaye alikuwa akishiriki kutoka wilaya ya Kishapu  baada ya kushindanishwa  washiriki 15  kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya za mkoa huu.

Mshindi huyo ametangazwa   rasmi tarehe 11/10/2026  na Asela Magaka  ambaye  alikuwa moja wa majaji wa shindano hilo   akiongozana na majaji wengine watano  huku Mshindi wa pili  akichukuwa  Editha Shushu kutoka Ushetu na mshindi wa tatu  ni Regina Mashimba kutoka Mjini Shinyanga.

Pia  Mshindi wa  Top Model  ametangazwa kuwa ni    Fafswa Suleiman  na   Regina  Mashimba  ametangazwa kuwa  Mshindi   ambaye chagua la watu  kupitia mtandaoni.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Holysimile Anord  Bweichuma ameeleza  majaji kuwa na vigezo vyao  vya kumpitisha  mshindi ingawa  washiriki wote ni washindi wanastahili  huku akieleza  jitihada  binafsi za kufanikisha shindano la Miss Shinyanga ambayo  pia imekuwa ni kazi kubwa kwa wadhamini  kujitokeza.

Bweichuma amesema   mashindano haya  yalikuwa yakiendeshwa nchini Tanzania na mkoa wa Shinyanga  pia yalikuwa yakifanyika na mara ya mwisho yalifanyika mwaka 2024 na baadaye kusimama  lakini yametangazwa tena Taasisi ya Holysimile ikaona ni vyema kushika usukani huo  kutafura Miss Shinyanga na amepatikana.

“Mshindi wa taji la Miss Shinyanga ataungana na  mshindi wa pili na watatu  kwenda kushiriki mashindano ya  kumtafuta Miss kanda ya ziwa (Lakezone) kwa  kushirikisha mikoa sita ya kanda ya ziwa na baadaye mshiriki akipatikana huko atakwenda kushiriki Miss Tanzania hivyo wakazi wa mkoa wa Shinyanga nikuungana na washindi hawa kuwasaidia ili kuweza kutimiza ndoto zao za ushindi”.

Bweichuma amesema  kazi aliyokuwa nayo ya kumtafuta Miss Shinyanga imekwisha  kulikuwa na washiriki 15 wamechujwa kwa vigezo  nakubaki washiki nane ambao wamepata jukwaani   na majaji wamefanya kazi yao kwa kutumia vigezo walivyoviweka  ila amemuomba   Asela Magaka  kuwa mlezi wa   washindi  hao hata pale  wanapokuwa kambi ya kusubiri kwenda mkoani Mwanza  kwenye mashindano ya kanda ya ziwa.

Asela Magaka  ambaye amekubali kuwa mlezi katika  washiriki hao  baada ya kupatikana mshindi wa Miss Tanzania  alitoa ushauri  na wito kwa walimbwende hao kuwa kipindi hiki ni kipindi cha utandawazi tofauti na kipindi alichokuwa yeye muandaaji wa mashindano haya ngazi ya mkoa  na mshindi wa taji la Miss Temeke mwaka 1996.

“Nina washauri epukeni sana tabia zisizo faa kwenye jamii mtachafua taswira ya   mashindano ya Miss na mkoa kwa jumla mkajitunze nakuwa  mabinti wema kupitia ushiriki wenu mtajulukana na mtafanya kazi nyingi na  wasichana wengine watawaona nakujifunza kupitia kwenu mkawe viongozi wazuri nakutangaza mkoa”amesema Asela.


Mkuu wa wlaya ya Kishapu  Peter Masindi ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Mboni Mhita amepongeza Taasisi ya HolySimile kwa kufanikisha  amesema mashindao hayo jamii iondoe dhana ya kusema ni uhuni kwani wasichana wanajipatia fursa ya kwa nyanja nyingine  kusonga mbele ikiwemo ajira  ingekuwa ni uhuni hata serikali isingeshiriki kuhamasisha  suala hili Mashindano haya.

“Ninawaomba wazazi wawaachie mabinti wanaoweza wenye vipaji wajitokeze huwezi  jua kupitia mashindano haya akawa  tajiri mwenye sifa kubwa na kuweza kutoa ajira kwa mabinti wenzake msifikirie kwa mtazamo hasi dunia ya sasa imebadilika”amesema  Masindi.

Mshindi  wa taji la Miss Shinyanga Nura Justus  amesema  anawashukuru walimu na walezi  kwenye shindano hilo na wazazi wake kumtunza vizuri anaahidi kufanya vizuri  kuutangaza mkoa huu kwa rasilimali zilizopo na kuwaelimisha wasichana wenzake.


Post a Comment

0 Comments