MRADI wa ujenzi wa barabara kutoka Kahama Manzese hadi Kakola kata ya Bulyanhulu yenye urefu wa kilomita 73 umeweza kuleta mafanikio ya kutoa ajira 460 kwa Raia wa Tanzania na Raia wa kutoka nchini china.
Hayo yamesemwa leo na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Wakala ya Barabara Tanzania (Tanroads) Mhandisi Marco Bee alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliotembelea kwenye eneo la mradi huo ulioanza rasmi kutekelezwa mwezi Juni mwaka 2024 nakutarajia kukamilika mwezi Desemba mwaka 2026.
Mhandisi Bee amesema mradi huo umeleta mafanikio makubwa baada ya kuanza utekelezaji wake mojawapo ni utoaji wa ajira rasmi 460 ikiwa raia wa Tanzania ni 418 na raia wa kutoka nchini china ni 42.
“ Ajira zisizo rasmi zimepatikana kwa mama lishe ambapo wamekuwa wakikuza uchumi wao kwa namna moja au nyingine ikiwemo kuwapikia chakula wafanyakazi wa mradi huo”amesema Mhandisi Bee.
Mhandisi Bee amesema barabara hiyo imeanzia eneo la Kahama Manzese ambapo imekamilika kilomita 36 mpaka sasa na wanategemea mradi huu ukikamilika watanyanyua shughuli za kiuchumi na usafirishaji kuwa rahisi na wataweka taa maeneo yenye makazi ya watu.
Bee amesema eneo la Segese ni katikati ya barabara hii ambapo kutawekwa taa na mpaka kufikia hapo kipande kimekamilika bado kuweka marembo ya alama ikiwa Kalvati za boksi 14 zimejengwa sawa na asilimia 100 na pipe Kalvati 148 na kunyanyua matuta kwa kiwango cha juu kwaajili ya kujihami na madhara ya kukwama maji kipindi cha mvua hasa kwenye mvua za El-nino.
Naye Mhandis Samson Mgina amesema Kipande kinachoendelea ni ujenzi wa tabaka la saruji na hatua inaelekea mwisho kuweka lami ambapo kutoka mwanzo hadi kufikia eneo hili la ujenzi wa tamabaka la juu ni kilomita 60 ingawa mradi wote mpaka sasa kwenye utekelezaji wake umefikia asilimia 89.
Mgina ameeleza eneo ambalo wanazalisha au kusaga mawe limegawanyika kwenye hatua nne ili kuweza kupata kiwango cha mawe au kokoto zinzotumika kwenye ujenzi wa barabara kwa kiwango wanachokitaka na kuna mtambo wa kusaga mawe na kuchanganya zenge na kazi inakwenda kwa haraka.
Hata hivyo mradi huo umefadhiliwa fedha kutoka Kampuni ya mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kushirikiana na serikali na watekelezaji ni China Construction Engineering Civil Company(CCECC).






0 Comments