HALMASHAURI ya Msalala mkoani Shinyanga imetoa shilingi Milioni 526 kwaajili ya kuwapatia vikundi 39 vilivyokidhi vigezo huku wakielezwa fedha hizo ziende zikatumike kama makubaliano waliyoafikiana wakati wa kuunda vikundi hivyo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Francis Mlacha alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi hundi kwenye vikundi hivyo huku akieleza vikundi vya wanawake vingi vimekuwa vikifanya vizuri wasiwasi zaidi upo kwenye vikundi vya vijana katika marejesho.
“Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu iliweka utaratibu wa fedha zitolewe kwenye vikundi na urejeshaji uwe bila riba nawapongeza vikundi hivi kupita kwenye hatua ya kwanza hadi hii ya kuzipata fedha mkajikomboe kiuchumi na msibadilishe matumizi ya fedha hizo”amesema Mlacha.
Mbunge wa jimbo la Msalala Mabula Magangila amesema fedha hizo za mikopo zimetokana na ukusanyaji wa ushuru ushauri wananchi waendelee kubuni miradi mikubwa hata ya kuanzisha viwanda vidogovidogo nafasi hiyo wanayo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Mibako Mabubu alisema wamekuwa wakijitahidi kukusanya mapato na kuhakikisha kitu cha kwanza lazima watoe fedha za asilimia 10 ili liweze kufikia lengo na kiasi kinchotolewa leo ni robo ya kwanza ya mwaka wa fedha.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Husna Toni amesema wakati wa kuchukua mkopo kunakuwa na ushirikiano kwenye kikundi lakini wakichukua ukafika muda wa marejesho ushirikiano unapotea pia fedha za mkopo sio za kubadilishwa matumizi ndiyo maana baadhi yenu mmekuwa mkishindwa kwenye marejesho.
Ofisa Maendeleo ya Jamii Halmshauri ya Msalala Judica Sumari amesema mwaka wa fedha 2026/2027 halmashauri imepanga kuchangia zaidi ya shilingi Milioni 831.3 na hadi kufikia tarehe 25/10/2026 zaidi ya shilingi Milioni 256.5 tayari imekusanywa nani miongoni wa fedha ndani ya mkopo unaotolewa leo.
“Shilingi Milioni 526 zimeizinishwa kutolewa kwenye vikundi 39 ikiwa vikundi vya wanawake 16,vikundi vya vijana 15 na vikundi vya watu wenye ulemavu nane”amesema Sumari.
Sumari amesema wanaendelea na ufuatiliaji wa madeni chechefu kutoka kwenye vikundi vilivyowahi kunufaika na mikopo ya asilimia 10 ikiwa bado zaidi ya shilingi Milioni 537.3 zinadaiwa kutoka kwenye vikundi 74 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Baadhi ya waliopata mikopo ya halmashauri Lucas Makerezi na Rebeka Daudi kwa nyakati tofauti wamesema watakwenda kutumia kama walivyoomba madhumuni yake bila kubadilisha ili wafikie malengo.






0 Comments