WAZIRI GWAJIMA AMESEMA PJT- MMMAM BILA USIMAMIZI IMARA NI KAZI BURE

Na Kareny Masasy
Dodoma

PROGRAMU  Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ( PJT-MMMAM ) inayotekelezwa kwa sasa bila maafisa Ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii kuwa imara katika utekelezaji wake ni kazi bure.

Hayo yamesemwa leo  na Waziri wa Maendeleo ya Jamii,jinsia,wanawake  na Makundi Maalum Dk Dorothy Gwajima alipokuwa  akifungua    kikao cha kutathimini  utekelezaji nusu mwaka wa programu hiyo kwa washiriki wa sekta mbalimbali za serikali na mashirika ya watu binafsi na kundi la waandishi wa habari.

Dk Gwajima amesema  mpango wa lishe nchini Rais  Samia Suluhu Hassan alisisitiza  kuweka mkataba kuanzia ngazi ya  mkoa hadi kata na halmashauri kufikia maazimio ya kutenga shilingi 1000  jambo ambalo hilo amelipongeza kwa kufanikiwa vizuri.

Dk Gwajima amesema  mpango kazi ulipishwa wa uendeshaji  kwenye jamii  (Social work  care oparetion) na  umeshindwa kuusimamiwa na wanaouangusha ni wale waliokubaliana  awali hivyo atarudi tena mezani kuzungumza na waziri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa (tamisemi) kwaajili ya kurudisha mpango huo nakusimamiwa vizuri.

"Ninaomba makatibu tawala mikoa yote waendelee kufahamu programu hii tuweze kunusuru kizazi hiki katika malezi na maadili tunashikiru mtu wa nje kutuletea kwaajili ya kutufungua bongo zetu  kwani kufanya hivyo ametupendelea jukumu hili lilitakiwa tulifanye wenyewe kuanza mapema jukumu hili watoto wakiwa bado wadogo"amesema Dk Gwajima.

Dk Gwajima amesema  viongozi walipo na kujielewa ni neema waliyoipata kutoka kwa wazazi na jamii  kwa sasa ilipofikia inatakiwa ipewe uelewa juu ya malezi na makuzi kwa watoto wao.

"Hali ilivyo kwa sasa  kutokana na kizazi ambacho hakijakuwa kwenye ukuaji uliotimilifu  utakuta wazazi walipenda na baadaye kuhitilafiana watoto waliowazaa wanaanza kuzagaa mitaani nakukosa malezi,pia utakuta mtumishi  yuko na simu, kinachoendelea kwenye mitandao ni ukosefu wa maadili ndiyo tulipofikia tuanze sasa kujenga kizazi chenye uelewa kuanzia malezi,makuzi na maadili" amesema dk Gwajima.

Post a Comment

0 Comments