MGODI WA DHAHABU BULYANHULU KILA MWAKA HUTOA BILIONI MBILI KWENYE CSR

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, Ajira na Mahusiano Evaline Munisi ameieleza Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi wa   Maendeleo ya jamii kuwa mgodi wa dhahabu wa  Barrick Bulyanhulu  kila mwaka hutoa shilingi bilioni mbili  kwa ajili ya kurudisha faida kwa jamii (CSR) 

“fedha hizo zimetumika kwa ujenzi wa vituo vya afya, shule za msingi na sekondari pamoja na chuo cha ufundi stadi (VETA).

 Munis amesema hayo leo alipokuwa akitoa taarifa kwenye kamati hiyo chini ya mwenyekiti  wake Hawa  Chikoma  ambapo amesema  wafanyakazi 7,000 wamepimwa afya zao na katika kulinda usalama wa wafanyakazi kuna matumizi ya teknolojia katika uchimbaji wa madini.

 Mbunge wa jimbo la Temeke Mariam Kisangi ameomba uongozi wa mgodi kuwapa nafasi watu wenye ulemavu katika utoaji wa ajira pamoja na kuwapa elimu ya kanuni za afya na usalama mahali pa kazi,

“Kwa sababu katika taarifa iliyosomwa sijasikia sehemu ambayo imewagusa watu wenye ulemavu, niwaombe mtupe nafasi watu wenye ulemavu katika CSR mnazofanya na nafasi za ajira katika mgodi huu nasi tuweze kukua kiuchumi” alisema Munis.

Hata hivyo Meneja mahusiano na mazingira mgodi wa Bulyanhuru Agapith Paul amesema  Kuna shule ya msingi imejengwa kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu inaitwa Segese  kuna mazingira yaliyoweka pamoja na vifaa vya walemavu katika hali ya usalama.

Mwenyekiti Hawa Chakoma ambaye pia ni mbunge wa viti maalum, ameridhishwa na utekelezaji wa kanuni za afya na usalama katika mgodi wa Bulyanhuru uliopo Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
“Tunapenda kuona watumishi wote wanajengewa uwezo na watumishi wote wanapatiwa mafunzo ya usalama mahali pa kazi pia hongereni kwa kuweka ushirikiano mwema na vyama vya wafanyakazi pamoja na kuona jamii zinanufaika na mgodi"amesema chikoma

 Chikoma amesema  kamati inasisitiza kuendelea kushirikisha jamii katika miradi na kufuata utaratibu kama ambavyo sheria inahitaji.

Post a Comment

0 Comments