Katika
ziara hiyo, Mhe. Rais Samia amepongeza PSSSF kwa kushiriki katika
maonesho hayo na kutoa huduma pamoja na elimu kwa wanachama na wananchi
wanaotembelea banda la Mfuko.
Mhe.
Rais Samia alipokelewa na Meneja wa PSSSF Ofisi ya Zanzibar, Bi. Mariam
Saleh, ambaye alimueleza kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko, pamoja na
namna wanachama na wananchi wanavyonufaika na huduma hizo kupitia banda
hilo.
Mhe. Rais Samia ameupongeza Mfuko kwa utoaji wa huduma na kusisitiza umuhimu wa kusikiliza na kushughulikia kwa wakati changamoto zinazowasilishwa na wananchi na wanachama.
“Nawapongeza sana kwa huduma nzuri. Kama kuna malalamiko, yakusanyeni na muyafanyie kazi,” ameagiza Mhe. Rais Samia.
Ushiriki wa PSSSF katika Tamasha la Kizimkazi unalenga kuendelea kuwafikia wanachama na wananchi kwa kuwapatia elimu kuhusu hifadhi ya jamii, huduma zinazotolewa na Mfuko pamoja na kuwawezesha kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu mafao na huduma za PSSSF.

0 Comments